Header Ads

Responsive Ads Here

MAHAKAMA YA TANZANIA YAPOKEA LESENI YA KIBALI CHA UCHAPISHAJI WA JARIDA LAKE LA HAKI BULLETIN


DSC00653
Msajili Mkuu (kulia) akionesha leseni hiyo kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa tayari kwa kuanza rasmi uchapishwaji wa Jarida la Mahakama. Lengo la Jarida hilo litakalokuwa likiandaliwa na Kitengo cha Habari, Elim na Mawasiliano kwa ushirikiano na Bodi ya Uhariri-Mahakama ni kuuhabarisha Wananchi na Wadau wake juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea ndani ya Mahakama. Jarida hili litakuwa likipatikana pia ‘online

DSC00656
Wakifurahia kwa pamoja mara baada ya kukabidhiwa leseni hiyo.
DSC00660
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania,  Mhe. Katarina Revokati (kulia) akikabidhiwa leseni ya uchapishaji wa Jarida la Mahakama kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi-Sehemu ya Usajili wa Magazeti, Idara ya HABARI-MAELEZO, Bw. Patrick Kipangula (wa pili kushoto), wanaoshuhudia zoezi hilo ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe (wa pili kulia) na wa kwanza kushoto ni Bw. Samson Mashalla, Mtendaji wa Mahakama, anayeshughulikia Mahakama Kuu ambaye pia ni Mjumbe ya Bodi ya Wahariri (Editorial Board) ya Jarida la Mahakama lijulikanalo kwa jina la ‘HAKI BULLETIN’ linalotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
Picha na Mary Gwera, Mahakama

No comments