Header Ads

Responsive Ads Here

KWA MARA YA KWANNZA WIZARA YA MADINI KUFANYA MNADA WA TANZANITE MIRERANI


picha 1
Madini ya Tanzanite yakipimwa kabla ya kuanza kufanyiwa mnada.

PICHA 2
Vifaa maalum( drum) vilivyohifadhia madini ya Tanzanite.
PICHA 3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa , John Nayopa ( aliyesimama)akifatilia zoezi la uthaminishaji, uchambuzi,na ukokotoaji wa mrabaha wa madini yaliyoletwa kwa ajili ya mnada, linalofanywa na watendaji wa Wizara ya Madini.
PICHA 4
Vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na watendaji wa Wizara ya Madini wakihakikisha usalama wa Madini ya Tanzanite yaliyohifadhiwa katika vifaa maalum.
picha 5
Usajili wa washiriki wa mnada wa madini ya Tanzanite ukiendelea mkoani Manyara.
……………..

Na Zuena Msuya, Manyara
Wizara ya Madini kwa mara ya kwanza itafanya mnada wa madini ya Tanzanite kutoka  katika Kampuni nne za uchimbaji na biashara ya madini katika eneo la Mirelani wilayani Simanjiro mkoani Manyara,Mnada huo utafayika tarehe 15, Octoba mwaka huu mkoani Manyara.
Akizungumza mkoani Manyara, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uchumi na Biashara ya Madini, Godleader Shoo alisema kuwa utaratibu  wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.
Shoo alifafanua kuwa mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo atakayefanikiwa kununua madini hayo katika mnada huo ni yule tu atakayeshinda bei iliyowekwa kwa ajili ya kununua madini husika.
Alitaja kampuni zitakazouza madini katika mnada huo kuwa ni Kampuni ya uchimbaji madini ya TanzaniteOne, Franone, Glitter Germs pamoja na Classic Gems ambazo zitazouza madini ghafi na yale yaliyokatwa.
Akizungumzia mnada huo, Shoo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO), Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro pamoja na Wizara ya Madini, ili kuhakikisha kuwa wauzaji na wanunuzi wa madini hayo wanapata kile wanachostahili.
”  Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwani Madini ya Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hili ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,” alisema Shoo.
Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki  na kodi nyingine za serikali kwa uwazi ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao.
Alisema kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya Vito kama vile Zambia( emerald), Zimbabwe ( Almasi) pamoja na Afrika kusini ( Almasi).
Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Octoba 15 mwaka huu  mkoani Manyara.

No comments