Header Ads

Responsive Ads Here

Kuelekea siku ya kumbukumbu ya Baba wa taifa Dc Sofia Mjema awaongoza mamia ya vijana wa UVCCM wilaya ya ilala katika zoezi la kufanya usafi hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam

 

 
Mkuuwa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema  aliye vaaqkilemba ,aliye upande waq  kushoto ni Diwani wa kata ya Ilala  Mhe. Saad Kimji akifagia na vijana wa  Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Ilala  katika Hospital ya Mnazi mmoja  jijini Dar es salaam leo katika kuelekea madhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Mwalimu JK nyerere.
 
Mmoja wa viongozi wa umoja wa vijana CCM ilala akimpati zawadi ya Sabuni mama mzazi Ruth Eliya  aliye jifungua jana katika Hospital ya mnazimoja ,aliye upande wamisho kulia ni Mkuuwa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema .
 

Diwani wa kata ya Ilala Mhe.Saad Kimji akizungumzaz na waandishi wa  habari baada ya zoezi la kufanya usafi  na kutoa misaada katika hospital ya mnazi mmoja 

 Katibu wa umoja wa vijana UVCCM  Wilaya ya Ilala Irene Moleli akizungumza na wana habari  baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi na kutoa misaada katika hospital ya  Mnazi mmoja , moja ya misaada ilitolewa hapo ni sabuni ya unga na sabuni za mche.


 Mganga mfawidhi wa Hospital ya mnazi mmoja Helman Ngonyani, akitoa neno la shukrani kwa  UVCCM na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kuhitika kwa ziara hiyo. Baadhi ya vijana  wa UVCCM  wakizoa taka  katika Hospital ya Mnazi mmoja , 

 Baadhi ya vijana  wa UVCCM  wakizoa taka  katika Hospital ya Mnazi mmoja , 
 
Na Mwandishi wetu Dar
 
Katika  kuazimisha siku ya kumbukumbu ya  kifo cha mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema leo ameongoza  umomoja wa Vijana CCM, Wilaya ya Ilala kufanya usafi na kugawa  misaada ya kijamii katika Hospital ya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza baada ya zoezi hilo Mhe. Mjema amesema , Wameamua kufanya usafi  na kugawa zawadi hizo ili kumuenzi Babawa Taifa na amewapongeza vjiana wote walijitokeza katika shuguli hiyo kwani nitendo la uzalendo amabalo linawafanya watu wengi kumkumbuka mwalimu Nyerere kwa uadilifu wake alivyo litumika Taifa enzi ya uhai wake.
 
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospital hiyo Helmani Gonyani, amewashukuru vija wa umoja huo kwa kutembelea hospitali hiyo na kufanya usafi na kuwataka tena iwapo wata pata nafasi siku nyingine wafanye hivo kwani wamefariji wagonjwa na kuhamasisha umoja wa kitaifa.
 
Naye diwani wa kata ya Ilala Saad Kimji akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa kata hiyo  ameushukuru uongozi wa hospital hiyo kwa mapokezi  na ushirikiano wa walioupata  katika hospital hiyo na kupongeza watumishi wote wa hospital kwa uzalendo wao na kutoa huduma kwa  , na kutoa wito kwa vijana wa Illala kuwa wazalendo kwa kufanya kazi za kijaamii bila kujali itikadizao  za kisiasa.
 
Irene Godfrey Moleli  ni katibu wa umoja wa vijina  wa wilaya ya Ilala , amesema , UVCC Wilaya hiyo  umeandaa bonanza  na ligi ya mpira kwaajili ya kumuenzi hayati Mwalimu Julias Nyerere ambapo itaanza  tarehe 21 hadi 28 mwezi kakatika jimbo la Segerea na amewakaribisha vijana wote kuhudhuri uzinduzi wa ligi hiyo na kushiriki michezo kwa muda wote wa ligi hiyo.

No comments