Header Ads

Responsive Ads Here

KESI YA MSUKUMA NA MADIWANI NANE YAPIGWA TAREHE


Mbunge wa Jimbo la Geita,na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita ,Joseph Kasheku(Msukuma) akiteta jambo  nje ya mahakama baada ya kesi kuhailishwa


Baadhi ya wananchi ambao walijitokeza kusikiliza kesi hiyowakiwa nje ya mahakama.         


 Picha na Joel maduka.
 
Kesi inayomkabili Mbunge wa Geita na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoani Geita
Joseph Kasheku Msukuma na madiwani nane imesogezwa mbele baada ya upande wa
mashitaka kudai upelelezi haujakamilika. 
 
 
Kesi hiyo ambayo ilikuwa isikilizwe leo imepangwa kutajwa tarehe 10 mwezi wa 11
mwaka huu ambapo washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana.
 
 
Kwa
upande wake wakili anayewatetea washitakiwa Bw Deo Mgengeli ameelezea hatua
ambayo imeendelea siku ya leo mahakamani hapo kuwa shauri limekuja na kwamba
limetajwa na hadi sasa hakuna mshitakiwa ambaye ameongezeka hivyo mahakama
imeamua tarehe Kumi mwezi wa 11 wawasili mahakamani kusikiliza tena kesi hiyo.
  
Aidha
wakili Mgengeli amezungumzia suala la madiwani wengine waliokamatwa na jeshi la
polisi na kutofikishwa mahakamani  amesema
kuwa kukamatwa  kwa madiwani hao  ni jambo la kawaida  kwani ni swala la upepelezi kwa makosa ya
jinai na kwamba alhamisi wanatakiwa kwenda tena polisi ili kujua ni kipi
ambacho kinaendelea ila hadi sasa awana kosa lolote.

 Awali washitakiwa hao kwa pamoja walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita Septemba 19 mwaka huu    Washitakiwa wanakabiliwa a mashitaka ya kufanya mkutano bila kibali, kuziba barabara na uharibifu wa bomba la maji linaloelekea kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM.
 
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE


No comments