Header Ads

Responsive Ads Here

KATIKA KUSHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA ‘STARTIMES YAZINDUA CHANELI MPYA’


IMG_5985
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kmpuni ya StarTimes ndg.Carter Luoh akizungumzana na waandishi wa habari ( hawapo pichani) katika kusherehekea Wiki ya Huduma ya Wateja.

IMG_5988
Meneja wa Uendeshaji Ndg Gaspa Ngowi kushoto akizungumzana na waandishi wa habari ( hawapo pichani) katika kusherehekea Wiki ya Huduma ya Wateja
IMG_5986
Meneja wa huduma kwa wateja ndg.Henry Ngailo akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari kulia katika kusherehekea Wiki ya Huduma ya Wateja.
IMG_5970
Technical Manager Tanzania wa StarTimes ndg Yusuph Baracha akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari kwenye studio ya kurushia matangazo katika kusherehekea Wiki ya Huduma ya Wateja.
Dar es Salaam.
IMG_5990
Katika kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi wa kumi, StarTimes imeongeza chaneli mpya kwenye king’amuzi chao. Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji Ndg Carter Luoh alisema kuwa wanajitahidi kusogeza huduma karibu zaidi katika Mikoa yote ya Tanzania.
IMG_5982
“Star  Media (T) Ltd ina furaha kubwa kuwa mtoa huduma za kidigitali anayeongoza Tanzania tukiwa  na zaidi ya wateja Milioni moja. Sasa zaidi ya Mikoa 17 imefikiwa na huduma yetu na hivi majuzi tumefikisha ving’amuzi Kigoma na Mtwara ikifatia. Yote bhii ni jitihada za kampuni katika kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya gharama nafuu kabisa anayoweza kumudu na pia ndoto yetu kufikia kila familia ya kitazania kupitia matangazo ya kidigitali. Katika kuhakikisha hili tunatoa huduma zetu kwa bei nafuu kabisa na kiwango cha hali ya juu” Alisema Ndugu Luoh.
IMG_6002
“Na sasa tunayo furaha kupanua zaidi huduma kwa wateja, tuna zaidi ya mawakala 300 katika kituo chetu cha simu ambao wapo tayari kutoa huduma muda wote kupitia namba 0764 700 800. Pia kufuatia malalamiko ya wateja wetu kuhusu kuongeza namba ya mtandao wa Tigo, Sasa tumeongeza namba 0677 700 800 ambayo itapatikana muda wote kama zilivyo namba zetu nyingine. Ukiacha watoa huduma kwa wateja  kwa njia ya simu, wateja wetu wanaweza kupata huduma ile ile kupitia ofisi zetu na mawakala wetu. Kwa kuongeza tunatoa huduma baada ya kuuza vifaa vyetu kupitia huduma ya mlango kwa mlango ambapo mafundi wetu huzungukia maeneo mbali mbali kufanya marekebisho kwa wateja wetu” Alihitimisha.
IMG_5988
Kwa upande wake Meneja wa Uendeshaji Ndg Gaspa Ngowi aliongezea, kwamba sherehe hizi zinaambatana na uongezwaji wa Chaneli Mpya kama vile ST Bollywood Africa,ST Bollywood na FOX Life huku nyingine zikiwa njiani.
IMG_5974
“Wiki ni ya kipekee sana kwa wateja wetu pendwa na tungependa kuwaonesha kwamba tunajali mchango wao mkubwa katika kampuni yetu na bidhaa zetu. Tukanona njia bora ya kusherehekea hii wiki ni kwa kutambulisah chaneli zetu Mpya katika king’amuzi chetu. Katika chaneli tulizoongeza kama vile ST Bollywood Africa ST Bollywood zitakuwa zikionyesha filamu kabambe za kihindi huku mteja mwenyewe atachagua lugha anayotaka, Kiswahili kikiwa ni mojawapo.
IMG_5958
Shindano la kuingiza Sauti sasa kuhamia Mwanza.
Baada ya Usaili wa Zanzibar kufanikiwa sana, Wikiendi hii usaili utakuwa jijini Mwanza ambapo watanzania wanapewa wito wa kushiriki Shindano hili ambalo litawapatia fursa ya kujipatia Ajira nchini China huku wakiwa Mabalozi wakubwa wa Kiswahili kimataifa.
Washishi wa mwaka jana tayari wako China wakiendelea na kazi yao ya kuingiza Sauti. Si hivyo tu pia walipata fursa ya kuhudhuria makongamano ya kimataifa yanayokutanisha tamaduni mbalimbali kutoka ulimwenguni kote.
Usaili jijini Mwanza utafanyika Jumamosi hii tarehe 7 mwezi wa kumi kuanzia saa tatu Asubuhi katika Viwanja vya Rock City Mall. Tunawakaribisha makampuni mbalimbali ambayo yangependa kutangaza nasi katika kipindi hiki cha Shindano, nafasi ya matangazo ni kubwa na wapokeaji ni wengi pia.
Meneja wa uendeshaji alimaliza kwa kutaja bidhaa nyingine Mpya ambazo zipo dukani kwa sasa kama vile Televisheni Mpya ya inch 42 na King’amuzi cha Combo ambavyo vyote vina ving’amuzi ndani.
Kama sehemu ya kusherehekea StarTimes ilitoa nafasikwa wateja kutembelea kituo cha Kupiga na Kupokea Simu (Call Centre Unit) ili kujionea namna maombi na mtatizo yao hushughuilikiwa kwa ustadi kabisa. Pia walipelekwa kwenye vyumba vya kurushia matangazo kujionea kwa macho.

No comments