Header Ads

Responsive Ads Here

KATIBU MWENEZI WA CCM MANISPAA YA IRINGA WAPINZANI MJIPANGE VILIVYO KUENDELEA KUWA MADARAKANI

 Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo sabasaba manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.

 
Katibu mwenezi wa chama cha
mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kujipanga
vilivyo kwa kuwa amechaguliwa kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi na wananchi
wa manispaa wanakuwa na imani na kukirudisha chama hicho madarakani katika
chaguzi zote zitakazo jitokeza hapo baadae.
 
Akizungumza wakati wa
kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Bashir
alisema kuwa atahakikisha anakieneza chama vilivyo ili kuongeza wanachama
wanaokipenda chama hicho.
 
“Mimi mwenezi hivi nilivyo
nitakieneza chama kwa nguvu zote kwasababu tunavijana na viongozi wa kuleta
mabadiliko ndani ya chama hata mkisema ninyoe nywele nitanyoa(hata wakisema
tumooge mafwiri tumoga eeela) kwa lengo la kuhakikisha tujakijenga chama kuwa chama
cha wananchi” alisema Bashir
 
Bashir aliwataka wanachama
kushikana kuahakikisha wanakuwa wamoja ili kuongeza wanacha wengine na
kuendelea kuimalisha jumuhiya zote za chama hicho za  manispaa ya Iringa.
 
“Bila kuwa na umoja hatuwezi
kwenda mbali wala kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mmenichagua kuwa
mwenezi hivyo nitaifanya kazi yangu kwa moyo wangu wote” alisema Bashir
 
Aidha Bashir aliwashukuru
wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa na imani naye na kuhakikisha
amekuwa mwenezi hivyo ametoa pongezi kwa wale waote waliomchagua kwa kura
nyingi.
 
“Mmenifanya niwe na furaha
sana maana sio kwa wingi wa zile kura mlizonipa
na kunifanya leo hii nasimama kama mwenezi kwa ajili ya kura zenu sasa
subirini kazi yangu ya kukieneza chama na naomba tusahau yote yaliyopita na
kuhakikisha tunaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Bashir
 
Naye katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marko Mbago alimpongeza Edwin Bashir kwa
ushindi alioupata na kumuomba kukieneza chama kwa nguvu zote hata kwa kuutumia
umaarufu wake kuongeza wanachama ambao watakitumikia chama hiki hapa manispaa.
 
“Wewe ni maarufu na
unapendwa sana hivyo tunatengemea mengi kutoka kwa kutokana na uzoefu wako wa
kuishi vizuri na wananchi wa manispaa ya Iringa na kuijenga CCM mpya hapa
manispaa” alisema Mbago
 
Kwa upande wake mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa sasa ni
muda mwafaka wa kuongeza wanachama wapya na kuimarisha jumuhiya zote hapa
manispaa ili kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi ya kushinda tena.
 
“Mimi nakufahamu muda mrefu
sasa tumia vijana wako wote ambao umewapa mafanikio kwa muda mrefu kukurudisha
fadhila na kukuunga mkono katika harakati zako za kisiasa” alisema Rubeya
 
Ritta Kabati ni mbunge wa
viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alimpongeza
mwenezi Edwin Bashir kwa ushindi alioupata lakini akawataka viongozi wengine
kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika haraka zake za kueneza chama.
 

“Kufanya kazi pekee yake
hawezi kupata matokeo chanya hivyo ni lazima sisi viongozi na wanachama kumpa
ushirikiano wakutosha kuhakikisha mikakati yake inaenda vile chama kinataka na
kuahikisha anaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Kabati

No comments