Header Ads

Responsive Ads Here

JUBILEE YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI SHINYANGA 'SHY BUSH' KUFANYIKA OKTOBA 13,2017

SeeBait

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab TelackA akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 6,2017-Picha na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Jubilee ya Miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga “Shy Bush” iliyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga inatarajia kufanyika Oktoba 13,2017 katika shule hiyo.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari leo,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack amesema Jubilee hiyo itahudhuriwa na watu mbalimbali waliosoma katika shule hiyo na sasa wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali.

“Hii ni shule ya sekondari kongwe zaidi mkoani Shinyanga yenye kidato kwanza hadi cha sita,tutafanya Jubilei ya miaka 50,siku hiyo itahudhuriwa na waliokuwa viongozi wa shule,wahitimu wa shule hiyo na watu wengine mbalimbali”,alieleza Telack.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwaalika wahitimu wa shule hiyo na wananchi kwa ujumla kuhudhuria katika Jubilei hiyo.

No comments