Header Ads

Responsive Ads Here

JAMII YAASWA KUENDELEA KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI GEITA


Watoto wa kituo cha kulelea watoto ambao wanatoka kwenye mazingira Magumu Mkoani Geita cha Brith Light wakiwa kwenye sherehe ya chakula cha mchana pamoja kuchangia mahitaji mbali mbali ambayo yanawakabili kituoni hapo.


Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mkoani Geita Robart Ngai akisisitiza watu kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea kuwasaidia watoto ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za kielimu pamoja na maradhi ili kujenga Taifa la kesho ambalo litakuwa na Elimu.

Watoto wa kituo cha Brith Light wakiimba wakati wa sherehee za chakula cha mchana.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wakiendelea kufuatilia na kusikiliza kwa umakini kile ambacho kilikuwa kikiendelea meza Kuu.

Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Brith
light  Methiw Daniel akisisitiza jamii kuendelea kuwaona watoto ambao wanaishi mazingira Magumu kuwa ni mtoto wa kila mtu na kwamba wajibu wa kuwasaidia na wa kila mwanajamii.


Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ualbino Mkoani Geita,Isaack Timothi amewahasa wananchi
Mkoani Geita kuwa na mwitikio wa kuwasaidia watoto na kuachana na maswala ya
ubinafisi.


Ayoub Ambaye anatoka taasisi ya marafiki wa Elimu akielezea mikakati ya kuendelea kushirikiana na taasisi Hiyo ambayo imejitolea kuwasaidia watoto wanatoka mazingira magumu.


Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye alitarajia kuwa mgeni rasmi kwenye hafra ambaye ni  ,Afisa maendeleo ya Jamii halmashauri ya mji wa Geita ,Bi Mariam John akielezea  mikakati ya serikali kusaidia kituo hicho.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoani Geita Victor Bariety akikabidhi katoni za sabuni ambazo zimetolewa na chama hicho.

Watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Brith Light wakisalimiana na Mgeni Rasmi pamoja na wagenu wengine ambao walikuwa meza Kuu.

Watoto pamoja na wageni waalikwa  na mgeni rasmi wakipiga picha ya pamoja.
PICHA NA JOEL MADUKA.

No comments