Header Ads

Responsive Ads Here

JAMII ISAIDIE KUTATUA TATIZO LA UGONJWA WA MDOMO SUNGURA


1
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura wakati wa siku ya “Smile day” kwenye hospitali ya CCBRT ya jijini. anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans

2
Mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura wakati wa siku ya “Smile day” akishiriki katika siku hiyo.
3
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na wazazi na watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura.
4
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na wafanyakazi wa hospitali ya CCBRT wakati wa siku ya “Smile day” iliyofanyikia kwenye hospitali hiyo.
5
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na mmoja wa watoto alyetibiwa na kupona ugonjwa wa ugonjwa wa midomo sungura.Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa hospitali ya CCBRT Brenda Msangi.
Picha|Mpiga picha wetu
………….
Na Mwandishi wetu
Miss Universe Tanzania ambayo uandaliwa na kampuni ya Compass Communications chini ya mkurugenzi, Maria Sarungi Tsehai, Jihan Dimachk ameiomba  jamii kusaidia watoto wanaosumbuliwa na
ugonjwa wa midomo sungura (Mdomo wazi) kupata  matibabu yanayofaa.
Jihan alisema hayo wa maadhimisho ya “Smile day” katika hospitali ya CCBRT ya jijin kwa kushirikiana taasisi ya Smile Train Africa linalojishughulisha na  utatuzi wa tatizo la mdomo sungura.
Jihan ambaye ni balozi wa shirika hilo alisema  kuwa jamii inatakiwa kuwakubali na  kushirikiana katika kutatua tatizo hilo ambao linawaathiri sana watoto wadogo.
Alisema kuwa taasisi ya Smile Train Africa linatambua tatizo la ugonjwa huo kwa watoto  ambao ukosa raha katika kula na kufanya mambo  mengine muhimu.
“Nimefarijika sana kuwa balozi wa Taasisi ya Smile Train Africa na hasa katika kuondoa  tatizo la ugonjwa wa Mdomo Sungura, naomba  Jamii iunge mkono juhudi za taasisi hii  kwani jukumu letu sisi,”
“Ugonjwa huu upo mikoa mingi na watoto wanahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji na  gharama za matibabu na gharama ni kubwa, nimeguswa sana na tatizo hili, ” alisema.
Taasisi ya Smile Train Afrika hutoa msaada wa kifedha na vifaa ili  kusaidia kufidia gharama kwa ajili ya upasuaji. Uwekezaji wote huu si tu kwamba  unawezesha upasuaji mkubwa lakini pia unafanya  upasuaji huu uwe salama na wa ubora wa hali ya  juu.

No comments