Header Ads

Responsive Ads Here

IGP SIRRO ATOA WITO KWA WANASIASA


5 (2)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, ametoa wito kwa wanasiasa kutokuliingilia Jeshi la Polisi na kuliacha liendelee na kazi zake za uchunguzi na kuhakikisha suala la usalama wa raia na mali zao unazidi kuimarika.

IGP Sirro, ameyasema hayo akiwa mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi ya siku moja ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kusema suala la Uchunguzi na Upelelezi ni jukumu la Jeshi la Polisi.
Pia amewaasa wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kujihusisha na vitendo vya mauaji kwa imani za kishirikina na badala yake wawe raia wema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua wahalifu.

No comments