Header Ads

Responsive Ads Here

HALMASHAURI ZENYE MADENI BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA ZATAKIWA KUREJESHA


1

Nteghenjwa Hosseah -TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zilizokopa Fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kutoka kwenye Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kuhakikisha wanarejesha fedha hizo kabla ya Disemba 2017.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na waandishi wa habari kuhusu marejesho ya mikopo kutoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na namna ambavyo Bodi hiyo inavyotakiwa kufanya kazi.
“Japo halmashauri nyingi zimejitahidi kurejesha Mikopo lakini kuna Halmashauri 9 zimeonyesha usugu uliopitiliza katika kurejesha Mikopo hiyo ambazo zina jumla ya deni la zaidi ya Shilingi bilioni 2 na kitendo cha usugu katika urejeshaji wa mikopo kinanyima fursa kwa Halmashauri nyingine kupata mikopo.” alisema Jafo.
Halkadhalika Waziri Jafo alimuagiza Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Richard Mfugali kuacha kukaa ofisini na kuzitembelea halmashauri zote zinazodaiwa kwenda kukusanya madeni madeni hayo haraka ili Taasisi hiyo iweze kutekeleza majukumu yake na mikopo iendelee kutolewa kwa halmashauri nyingine zenye mahitaji.
Pia Mhe. Jafo ameielekezea Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kutoa Mikopo katika Halmashauri zinazolenga kutekeleza miradi ya viwanda na uwekezaji mdogo na mkubwa ili kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. .
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya  Shilingi bilioni 9.742 hadi Septemba 30,2017  kwa halmashauri 54 kati ya 185 zilizopo hivi sasa.
TAMISEMI YA WANANCHI

No comments