Header Ads

Responsive Ads Here

GORA MWENYEKITI CCM WILAYA KONDOA ILA UCHAGUZI WAGUBIKWA NA RUSHWA

Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Mwenyekiti wa CCM aliemaliza mda wake Othman Gora ametetea kiti chake baada ya kuwabwaga wagombea wenzake kwa kura 676 sawa na asililimia 76 ya kura zote 1092 zilizopigwa katika uchaguzi ambao siku mbili kabla ya uchaguzi huo viongozi walionekana wakitoa rushwa za wazi kwa wajumbe ilikujipanga na uchaguzi mkuu 2020

Makundi ya uchaguzi huo ambao wajumbe walianza minong’ono kabla msimamizi wa uchaguzi huo hajatangaza matokeo, wapambe walianza kumtangaza mgombea Gora kuwa ameshinda bila kujali kanuni za uchaguzi ambapo hapo kabla ya kufika ukumbini wajumbe walionekana wakikaa vikundi na kupewa fedha kiasi cha Elfu kumi na kupewa maelekezo ya nani anaetakiwa. 
Wajumbe 1092 zaidi ya asilimia 98.99  ambao walishiriki kupiga kura, ambapo wagombea kwa nafasi mbali mbali walikuwa nafasi ya mwenyekiti wakiwa 3 nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu taifa wakiwa 9 na wajumbe halmashauri kuu wilaya wakiwa 6 na wajumbe nafasi ya uwt wilaya 7 nafasi ya wajumbe kutoka kundi la vijana wakiwa 7.
Akisoma matokeo hayo majira ya saa 7.15 usiku Msimamizi wa uchaguzi huo Mbunge wa Mtera na mjumbe wa halmashauri kuu taifa Job Lusinde alimtangaza Othman Gora kuwa mshindi wa kiti cha uwenyekiti wa wilaya hiyo kwa kuwabwa wenzake Kimolo Iddy na Juma Fataki.
Lusinde alisema kuwa uchaguzi huo ambao ulienda kwa uwazi na kuwapata viongozi hao ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano na kuwataka wale ambao kura hazikutosha wajipange kwa uchaguzi ujao na kuwa kitu kimoja katika kukijenga chama hicho.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa Othman Gora alisema kuwa ushindi aliopata ni wanaccm wote na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuimarika na kushinda chaguzi mbali mbali ikiwemo kuibua miradi ya maendeleo na kuisimamia serikali.
Kwa upande mwingine wajumbe wameulalamikia uchaguzi huo uliogubikwa na matukio ya rushwa za wazi wazi zikiongwa na naibu waziri wa fedha dakta.Ashatu Kijaji kwa upangaji wa safu yake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hali iliyopelekea wajumbe kupewa fedha wakitumia Makati wa ccm wa Kata na baadhi ya madiwani.
Hata hivyo baadhi ya wagombea wamekuwa wakiendelea na vikao vya chini kwa chini lengo likiwa ni kukata rufaa kwani uchaguzi huo kanuni na sheria zilikiukwa kwa kutangaza matokeo kabla ya msimamizi hajatangaza hali katika mkutano huo ambao uliendeshwa kwa uwazi lakini ukiwa na kasoro za upangaji wa matoke.
Pamoja na kuwepo taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU na kupewa taarifa za wazi bado hatua hazikuchukuliwa kwa wakati lakini mwanahabari hii juzi usiku katika kata ya Soera alishuhudia wajumbe wakipewa fedha na bwana aliefahamika kwa jina moja Ridhiwan.
Aidha pia huko kwenye kata za Bumbuta,Kisese,Kikore wajumbe walipewa mlungula wa wazi ambapo Naibu waziri alidai ametumwa na makamu wa Rais na mwenyekiti wa vijana kata ya Bumbuta Hemed alitishiwa kutolewa dirishani kwani ameonekana kumpinga Dkta Kijaji katika malengo yake.

No comments