Header Ads

Responsive Ads Here

Dkt. Ndungulile : Tujitokeze Kupima Afya Mara kwa Mara.


PIX 1
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndungulile akimpima mapigo ya moyo Sheikh wa Wilaya ya Kigamboni Ostadhi Abdallah wakati wa zoezi la upimaji afya lililoratibiwa na Taasisi za Afya P-Consultant Medical Clinic (PCMC) na Jamii Bora Haelth Services Network, zoezi lililofanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Jeshi la Wanamaji Kigamboni.PIX 2
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndungulile akipata maelezo kutoka kwa Wataalam wa dawa wa Hospitali ya P-consultant Medical Clinic (PCMC) wakati wa zoezi la upimaji afya bure kwa wananchi wa Wilaya ya Kigamboni pamoja na wananchi karibu ya maeneo hayo, zoezi lililofanyika Viwanja vya Hospitali ya Jeshi la Wanamaji Kigamboni.
PIX 3
Matroni  kutoka Jamii Bora Health Services Netwerk Fatma Awaph akimpima mmoja ya Askari wa Jeshi la maji katika zoezi la upimaji afya kwa wananchi Wilayani Kigamboni  Jijini Dar es Salaam mapema leo.
PIX 4
Fundi Sanifu Maabara Nasra Omary na Hazina Omary wakimpima mmoja wa wananchi waliojitokeza kupima afya zao katika zoezi lililofanyika Viwanja vya Hospitali ya Jeshi la Wanamaji Kigamboni.
Picha na Paschal Dotto-MAELEZO
……………………
Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleoa ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka wananchi kujitokeza kupima magonjwa yasiyo ambukiza ili kubaini haraka afya zao na kuchukua hatua za matibabu mapema endapo watagundulika kuwa na magonjwa hayo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Faustine Ndungulile katika zoezi la upimaji afya bure lililo ratibiwa na Taasisi binafsi za afya  hospitali za P-Consultant Medical Clinic (PCMC) pamoja na Jamii Bora Health Services Network katika viwanja vya jeshi Wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Ndugulile alisema kuwa katika hali ya sasa magonjwa yasiyo ambukizwa yamekuwa  yakipoteza maisha ya watu wengi sana  kwa hiyo kupima afya ni bora sana ili kujua afya,kwani  waswahili husema “kinga ni bora kuliko tiba” hii  itasaidia katika kujenga utamaduni wa kujua afya zao.
“Sasa hivi kama nchi kuna changamoto mbili kwanza magonjwa yanayoambukizwa na pili magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari, shininikizo la damu, kansa pamoja na kiharusi kwa hiyo watanzania wenzangu tupime ili kuyabaini mapema magonjwa haya na kuyadhibiti”,alisema Dkt.Ndungulile.
Alisema kuwa serikali ipo kwenye harakati ya kupunguza kwa kasi kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwani ni gharama kubwa, pia alibainisha kuwa magonjwa yanayongoza kwa kupeka watu nje ya nchi ni Kansa,  pamoja na Magonjwa ya mifupa.
Aliongeza kuwa kwa sasa hivi serikali ipo kwenye mkakati wa kuboresha huduma za afya kwa kuweka ubora wa huduma katika vituo vya afya, na mipango mbalimbali  ikiwemo upandikizaji figo, kuimarisha matibabu ya magonjwa ya moya pamoja na mifupa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Dkt.Ndungulile aliwashukuru wadau walioandaa zoezi hilo kuhamasisha wananchi wajitokeze katika upimaji afya bure ili kubaini afya zao mapema aliwasihi kuwahi mapema ili magonjwa hayo yaweze kudhibitiwa mapema.
Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa P-Consltant Medical Clinic (PCMC) Richard Ulanga  alisema kuwa zoezi hilo ni moja ya kuhudumia wananchi bure katika maeneo ya Wilaya ya kigamboni kwa hiyo wananchi katika maeneo hayo wajitokeze kwa wingi ili kupata huduma bora.
“Madaktari wakiona mtu anahitaji kupata vipimo zaidi tunamhamishia katika clinic zetu na kwa wale tutakaongundua  kuwa wana matatizo zaidi tutaendelea nao na gharama zitakuwa ni bure kabisa”, alisema Bw.Ulanga.

No comments