Header Ads

Responsive Ads Here

DK.KIKWETE -HALI YA MIUNDOMBINU KIBAHA SEKONDARI HAIRIDHISHI TUSHIRIKIANE KUITATUA


IMG_20170930_121715
Rais mstaafu wa awamu ya nne  dk.Jakaya Kikwete ,akitoka kutembelea bweni alikuwa analala wakati akisoma shule ya sekondari Kibaha mwaka 1966-1969, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo,huku akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa pili kushoto,na viongozi wa shule ya sekondari Kibaha na shirika la  elimu Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi)

IMG_20170930_131424
Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo maalum katika mahafali hayo.
IMG_20170930_133823
Rais mstaafu wa awamu ya nne  ,Dk.Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha aliyochorwa na mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne  shule ya sekondari Kibaha, Mkoani Pwani, wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne  shuleni  hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
IMG_20170930_135357
Rais mstaafu wa awamu ya nne  ,Dk.Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne  ya shule ya sekondari Kibaha mkoani Pwani ,shule ambayo aliwahi kusoma mwaka 1966-1969 .(picha na Mwamvua Mwinyi)
IMG_20170930_153809
Rais mstaafu wa awamu ya nne  ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne  shule ya sekondari Kibaha, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne  shuleni  hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Pic 4
Rais mstaafu wa awamu ya nne  ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Kibaha, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne  shuleni  hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Rais mstaafu wa awamu ya nne  ,dk.Jakaya Kikwete ,ametoa rai kwa wadau na viongozi ambao wametokea katika chimbuko la  shule ya sekondari ya Kibaha;” ,Kuangalia namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa ambayo inasababisha mlundikano wa wanafunzi madarasani.
Aidha amesema mbegu ya kuwa yeye mwanasiasa ilipandwa shuleni hapo, baada ya kuchaguliwa kiongozi wa baraza la shule kutokana na harakati zake za kutetea haki za wanafunzi .
Dk.Kikwete aliyasema hayo shirika la elimu Kibaha ,wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha ambako alipata elimu yake ya sekondari mwaka 1966 hadi 1969.
Alisema ,atashirikiana na wadau mbalimbali kuona namna bora ya kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la  upungufu wa madarasa .
Dk.Kikwete alisema , haipendezi na hajafurahishwa na hali ya miundombinu ilivyokuwa chakavu hali inayoathiri mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji .
Rais huyo mstaafu wa awamu ya nne  ,alieleza changamoto hizo si  sababu ya kushindwa bali  uwepo wa changamoto huongeza umakini ,bidii na ubunifu ili kukabiliana nazo .
Alifurahishwa kusikia serikali imejizatiti kukarabati shule kongwe nchini na shule ya sekondari Kibaha ikiwemo ,;”Hivyo aliwaomba wavute subira maana kulingana na kasi ya awamu ya tano anaamini ukarabati huo hautachelea .
Alielezea ,shirika la  elimu Kibaha ni chemchem ya elimu bora ,iliyozaa viongozi bora na wataalamu wanaoliletea sifa nzuri taifa  .
Dk.Kikwete alieleza kuwa ,pia shirika hilo ni tunu muhimu iliyoachwa na muasisi na baba wa taifa  mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na nchi za Nordic .
“Jamii ya watanzania inaendelea kushuhudia matokeo mazuri ya shule ya sekondari Kibaha katika mitihani ya kitaifa kwa kidato cha nne  na cha sita “
“Pia ushindi na tuzo katika nyanja zingine na mafanikio kwa wanajumuia ya shule hii ni ushahidi tosha kwamba ,shirika hili ni chemchemya elimu bora na iliyozalisha wanasiasa,madaktari,maprofesa ,wataalamu na viongozi wa juu” alifafanua dk.Kikwete .
Kuhusu miradi ya uzalishaji kwenye shirika hilo ,alisema ni wazo la  kulifanyia kazi ,itawasaidia kuwajengea vijana moyo  wa kupenda kazi za mikono na utakuwa  mtaji .
Dk.Kikwete, aliwatakia  wahitimu mafanikio mema katika mtihani wa kidato cha nne  kitaifa unaotarajiwa kuanza kufanyika octoba 30 mwaka huu .
Kabla ya shughuli ya mahafali hayo, alipata fursa ya kwenda kutembelea bweni alilokuwa akilala ,maktaba ,maabara  na maeneo mengine shuleni  humo  .
Awali mwenyekiti wa bodi ya shirika la elimu Kibaha, prof.Patrick Makungu ,alisema shirika linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia fani  za ufundi .
Alieleza ,shirika hilo ni taasisi ya kihuduma iliyoanzishwa miaka 54 iliyopita ,na jukumu lake kubwa ni kupigana na kushindwa maadui ujinga ,maradhi na umasikini .
Prof .Makungu alisema mkakati  wao ni kuhakikisha wanatoa wanafunzi na wanavyuo wenye maarifa ,ujuzi na nidhamu katika elimu ya msingi ,sekondari ,ufundi stadi ,mafunzo maafisa tabibu na uuguzi .
Nae mwalimu Mkuu shule ya sekondari Kibaha,Chrisdom Ambilikile alisema shule hiyo ipo  vizuri kitaaluma ambapo imekuwa ikifanya vizuri miaka 13 mfululizo sasa .
Alisema mwaka jana walipanda ufalu kitaifa kufikia nafasi ya 16 kutoka ya 69 hivyo wanatarajia kupanda zaidi .
Ambilikile alisema, wanatatizo la  upungufu wa madarasa matano ,ambao unasababisha mlundikano wa wanafunzi katika vyumba vichache vilivyopo .
Shule hiyo, ilianzishwa mwaka 1965  kwa msaada wa kifedha wa nchi za Nordic ikiwa  na wanafunzi 110  kwa sasa ina  wanafunzi 728 wote  wakiume ,walimu 57 ,Na wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne  mwaka huu  ni 116 .

No comments