Header Ads

Responsive Ads Here

CUF kusimamisha Wagombea Uchaguzi Mdogo wa Madiwani


Chama cha Wananchi (CUF) leo kimetangaza nafasi za wagombea wa ngazi ya madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara baada ya Tume ya Uchaguzi (NEC) kutangaza kuwa kampeni za Uchaguzi huo zitaanza tarehe 27 Octoba mwaka huu,


Akitangaza nafasi hizo za wagombea Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF Bw. Mneke Jafar amesema kuwa CUF imefanya upembuzi yakinifu kuhusu Uchaguzi huo na hatimaye kuamua kusimamisha wagombea kata zote 43 na maamuzi hayo yamezingatia msingi kuwa Watanzania wote wanahitaji haki sawa katika nyanja ya Kisiasa, Kiuchumi na mambo ya Kijamii.
“Tunapenda kuwataarifu Watanzania wote kuwa Chama chao cha Wananchi (CUF) kimwjipanga vizuri na kitasimamisha wagombea wazuri wenye uzalendo wa kweli wa kutumikia Watanzania katika kata zote 43, hivyo Chama kinawaomba Watanzania kujiandaa kuwaunga mkono wagombea hao watakao simamishwa na CUF mara baada ya uteuzi na Kampeni kuanza” Alisema Bw. Jafar.
Pia BwJafar alisema kuwa Chama cha CUF kimepokea na kinaendelea kupokea Wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali vya SiasaNchini, hiyo ikiwa ni ishara nzuri, njema ya matumaini makubwa waliyonayo Watanzania ya kupata ukombozi wa kweli chini ya Chama cha CUF.
Aidha aliwaomba Wanachama wa Cuf na Wananchi wote kupuuza propoganda za Wahafidhina waliofilisika kisiasa wanaopotosha Jamii kwa kauli za uongo na uchochezi kama vile “Yamebakimasaa machache kuapishwa“, “Wameshinda kesi” na kuwataka Wanachama na Watanzania wapuuze propaganda hizo chafu na badal yake waelekeze nguvu katika ujenzi wa Chama cha CUF.
Abdul Kambaya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari leo Makao Mkuu ya Chama Hicho, Buguruni.

No comments