Header Ads

Responsive Ads Here

BUNDALA AWEKA REKODI YA KUONGOZA CCM KIBAHA MJINI KWA AWAMU TATU MFULULIZO


SAM_6040
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MAULID Bundala ,amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)Kibaha Mjini ,kwa kupata kura 288 na kuweka rekodi ya kukiongoza chama wilayani humo kwa awamu tatu mfululizo .

Akitangaza matokeo katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa CCM wilayani hapo ,msimamizi wa uchaguzi huo Gama Juma Gama ambae pia ni katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoani Pwani ,alisema kura zilizopigwa zilikuwa 489.

Alieleza kwamba ,Bundala ameshinda dhidi ya wagombea wenzake Nyarusi John aliyepata kura 164 na Jabir Masenga kura 37 .

Gama alitangaza nafasi ya wajumbe watakaowakilisha mkutano mkuu Taifa kutoka CCM wilaya, kuwa ni AbdulAzizi Jadi kura 355,Catherine Katele kura 332 na Alice Kaijage kura 259 .

Nae katibu wa CCM Kibaha Mjini ,Abdallah Mdimu ,alieleza uchaguzi umekwenda vizuri kwa kufuata demokrasia .
Aliwataka wanachama wa chama hicho ,kwenda sambamba na mageuzi ya CCM mpya, ili kuendelea kushika dola katika chaguzi za serikali ya mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 .
Mdimu ,aliomba kuvunjwe makundi na kuwa wamoja ,pamoja na kuachana na tabia ya kuwekeana chuki na fitna zisizo na manufaa katika chama .
Awali mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,alisema kazi yake kubwa ni kusimamia ilani na kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo hivyo kwa kupata safu mpya ya viongozi kuanzia mashina ,matawi ,kata na wilaya itamsaidia kutekeleza ilani hiyo kirahisi .
Alielezea ,atahakikisha anashirikiana na viongozi hao kujenga na kutengeneza misingi mipya ya CCM mpya ,ili kutimiza madhumuni na azma ya mwenyekiti wa CCM Taifa dk. John Magufuli .
Koka ,alisema ni wakati wa kutoka kifua mbele na kuaminiwa na jamii kuwa chama kinatekeleza ilani na serikali yake ikiendelea kupambana na kuinua maendeleo na uchumi wa nchi kwa kasi kubwa .
Kwa upande wake Maulid Bundala ,alishukuru wajumbe waliomchagua na wasiomchagua na kuomba kuvunjwe makundi ili kuijenga Kibaha .
Alisema ni jukumu la kusimama kidete kuhakikisha chama kina simama imara na kudhibiti wapinzani wasiweze kupenya kwenye mbalimbali .
Bundala ,alisema anauzoefu kisiasa ,amepikwa kwa miaka mingi kuanzia jumuiya ya Vijana ,na uongozi katika nafasi mbalimbali za chama ,hivyo ataendelea kutumia uzoefu huo kukiimarisha chama hicho .
Alieleza kuwa , ufike wakati wa wanaCCM wilayani hapo kushikamana,na kuwa wamoja badala ya kutengana hali inayosababisha mipasuko isiyo na tija kwao .

No comments