Header Ads

Responsive Ads Here

BUMBULI WATAKIWA KUFUNGA NA KUTUMIA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI


1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo  akiwasili   katika  chuo cha Serikali za Mitaa – Hombolo kilipofanyika kikao cha uzinduzi wa  Baraza la wafanyakazi wa OR-TAMISEMI mapema leo.

2
Katibu Mkuu Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa OR-TAMISEMI kilichofanyika katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.
3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo  akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati wa Kikao cha uzinduzi wa  Baraza la wafanyakazi wa OR-TAMISEMI mapema leo.
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo akimkabidhi Mkataba wa kuunda Baraza la Wafanyakazi na Uendeshaji wa Vikao vya Baraza Mwenyekiti wa Baraza hilo  Mhandisi Mussa Iyombe wakati wa kikao cha uzinduzi wa  Baraza la wafanyakazi wa OR-TAMISEMI mapema leo.
5
Katika Picha ya Pamoja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za  Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(tano mbele) akiwa na viongozi na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi baada ya Uzinduzi wa Baraza hilo.
…………..

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga kuhakikisha inafunga na kutumia Mifumo fungamanishi ya Tehama iliyoko chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ifikapo Desemba 25, mwaka huu.
Waziri Jaffo alitoa agizo hilo wakati anazindua baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ofisi ya Rais – Tamisemi lilifanyika katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, mjini hapa.
Waziri Jaffo amelazimika kutoa agizo hilo baada ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhandishi Mussa Iyombe kuwasilisha Taarifa ya Utendaji Kazi wa Wizara iliyoainisha Halmashauri ambazo zimekwishafungiwa mifumo hiyo kuwa kati ya Halmashauri 185 ni Halmashauri 184 tu ndio zimefunga mfumo huo huku Bumbuli ikishindwa kufunga kutokana na kutokuwa na umeme.
Waziri Jafo alisema ameshangazwa na Halmashauri hiyo kutofunga mfumo huo hadi sasa kwa kisingizio kuwa hakuna umeme wakati zipo Halmashauri za pembezoni mwa nchi ambazo hazina umeme lakini zimeshafunga na zinatumia mfumo huo.
“Haiwezekani kushindwa kufunga mfumo kwa kisingizio cha umeme wakati Halmashauri kama ya Kakonko na kwingineko wamefunga mfumo huu na wanatumia,sitaki kuamini hii Bumbuli hata kununua genereta wameshindwa,”alisema Waziri Jaffo
Aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha inanunua genereta na kufunga mfumo huo kabla ya Desemba 25, mwaka huu.
“Wasipofunga walete taarifa kwa Waziri mwenye dhamana kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao, haiwezekani watu wamepewa dhamana hawatekelezi majukumu yao,”alisema Waziri Jaffo
Aidha alisema Wizara ya Tamisemi  kwasasa ni miongoni mwa taasisi tatu zinazofanya vizuri kwenye utendaji kazi tofauti na awali ambapo ilikuwa ikinyooshewa vidole kwa kukithiri kwa vitendo mbali ikiwemo vya rushwa.
Akizungumzia kuhusu mahusiano, Waziri Jaffo aliwataka wafanyakazi kuhakikisha wanakuwa na mahusiano mazuri kwenye utendaji kazi wao kwa kuwa kukosekana kwa mahusiano hakutakuwa na mafanikio.
“Utekelezaji wa bajeti unataka uwepo wa mahusiano mazuri na katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/18 muangalie namna mtakayofanya kuwepo na thamani ya fedha kwa kuwa asilimia 20.7 ya fedha za bajeti ya serikali zinakuja Tamisemi,”alisema Waziri Jaffo
Aliwataka watumishi wa Tamisemi kuhakikisha wanakuwa na utendaji unaoacha historia na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.
“Ofisi yahii tunapaswa kubadilika kwa kiwango kikubwa mmepata Waziri kijana lakini mwenye kasi katika utendaji kazi, mimi ni mzuri hapa mbaya pale kama huendi vizuri utaniona Jafo mbaya,”alisema Waziri Jaffo
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandishi Musa Iyombe alisema Wizara hii ndio inayoongoza kwa huduma za kielektroniki.
Aidha alisema watumishi 142 wameombewa kibali cha kupandishwa vyeo.“Katika zoezi la uhakiki wav yeti wafanyakazi wa wizara 12 tumewaondoa kwa kughushi vyeti na pia 19 wameondolewa kwa kukosa cheti cha kidato cha nne,”alisema Iyombe.
TAMISEMI YA WANANCHI

No comments