Header Ads

Responsive Ads Here

Benki ya Standard Chartered yadhamini kongamano la kimataifa la wanawake na fedha

 Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari.

Picha na Philemon Solomon.
,,,,,
Na Dotto Mwaibale

Benki ya Standard Chartered nchini, imedhamini kongamano la kimataifa la wanawake ambalo linatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na hapa nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani alisema kongamano hilo litakalowakusanya pamoja wanawake viongozi katika fani  mbalimbali zikiwemo za Mabenki, Teknolojia, Wafanyabiashara na Mashirika ya Umma na Mashirika binafsi litakuwa la siku mbili.

Rughani aliyeambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la 'Women's World, Banking na Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, alisema kuwa  benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuwawezesha wanawake kupata mitaji ya kifedha na kuwaelimisha wanawake kuhusu masuala ya  fedha na uchumi.

Aidha aliongeza kuwa, mambo mengine wanayowawezesha wanawake ni kutoa bidhaa maalum za kibenki  ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kupitia miradi yake ya kijamii.
"Wanawake wana mchango mkubwa katika maendeleo ya chumi za nchi na tumejizatiti kikamilifu kuwawezesha wanawake kuwa uhuru wa uchumi na fedha, kupata mitaji na kuwa na elimu ya mambo ya fedha na uchumi. Kama benki tutaendelea kumuwezesha mwanamke wa Kitanzania kuwa gurudumu la maendeleo la nchi yetu," alisema Rughani.

Rughani aliongeza kuwa, kongamano hilo litawahusisha wanawake 300 kutoka nchi mbalimbali duniani ambao wataongelea maudhui  yanayohusu kujumuishwa kwa wanawake katika mambo ya kifedha.

Washiriki watajumuisha viongozi wanawake wa sekta mbalimbali kama tekenolojia, uwekezaji,, viwanda, mabenki na mashirika ya kifedha pamoja na wanachama wa shirika la 'Women's Word Banking kutoka nchi 32.

"Benki ya Standar Chartered inaamini kuwa kongomano hili litaleta mageuzi ya kiuchumi na kuwawezesha wanawake kuwa wadau wakuu katika kuleta maendeleo nchini Tanzania na katika nchi mbalimbali ambazo zitashiriki," alisema Rughani.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la 'Women's World Banking', Tom Jones alisema washiriki mbalimbali kutoka sekta tofauti ni ushuhuda mkubwa kwamba wa jinsi ambavyo wanazidi kuchacharika katika kuleta maendeleo ya kiuchumi ya nchi zao.

Kwa upande wake, Bi Heidi Toribo ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya mabenki akizungumza na wanahabari waliohudhuria hafla hiyo alisema;

"Mwanamke anayejiweza kiuchumi anasaidia siyo tu biashara yake bali pia na familia yake kwani anakuwa ni mtaji mkubwa kwa jamii yake na kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla."

Kongamano hilo litafanyika wakati Benki ya Standard Chartered Tanzania ikiwa inaadhimisha miaka mia moja tangu ifungue biashara yake nchini Tanzania.

 Katika kuadhimisha mafanikio yake iliwakaribisha nchini zaidi ya viongozi 40 kutoka Mabara ya Afrika na Asia mwezi Machi mwaka huu. Viongozi hao walikutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, wateja, wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuthibitisha dhamira yake ya kuendelea kufanya biashara nchini kwa lengo la kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.

No comments