Header Ads

Responsive Ads Here

Benki ya NMB yaikabidhi Shule ya Msingi Karume vifaa vya ujenzi


Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Christine Lifiga (wa tatu kushoto) akimkabidhi Kaimu Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Bakari Mnondwa (mwenye miwani) mbao zilizotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya msaada wa mabati, mbao, misumari pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya kupauwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Karume vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Shule ya Msingi Karume ipo Kata ya Buza Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_82301" align="alignnone" width="500"]
Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Christine Lifiga (katikati) akimkabidhi Diwani Kata ya Buza, James Raphael (mwenye shati jeusi) mbao zilizotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya msaada wa mabati, mbao, misumari pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya kupauwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Karume vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano.[/caption] [caption id="attachment_82302" align="alignnone" width="500"]
Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Christine Lifiga (katikati) akiwakabidhi walimu wa Shule ya Msingi Karume baadhi ya mabati yaliotolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya msaada wa mbao, misumari pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya kupauwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Karume vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Shule ya Msingi Karume ipo Kata ya Buza Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam.[/caption] BENKI ya NMB imetoa msaada wa mabati, mbao, misumari pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya kupauwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Karume vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano ili kuisaidia shule hiyo kuondokana na msongamano wa wanafunzi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa. Akikabidhi msaada huo juzi, kwa niaba ya Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo, Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Christine Lifiga alisema msaada huo ni utaratibu wa kawaida ambao benki hiyo imejiwekea kurejea faida kiasi fulani wanayoipata kwa huduma anuai za kijamii ikiwemo elimu. Alisema NMB imeguswa na hali ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo na kuamua kutoa msaada huo utakaowezesha kukamilika kwa madarasa mawili yatakayopunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa. "...NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchangia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu pale inapokuwa na chochote," alisema Meneja huyo wa NMB Tawi la Temeke, Bi. Lifiga. Kwa upande wake Kaimu Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Bakari Mnondwa aliishukuru Benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia hali ya uboreshaji elimu maeneo mbalimbali ikiwemo katika shule za manispaa hiyo. "...Kweli nyinyi ni wadau muhimu wa maendeleo ya elimu, tunaomba muendelee kuwa na moyo huo huo wa kusaidia Serikali katika uboreshaji elimu. Serikali ina mzigo mkubwa haiwezi kuboresha kila jambo ndio maana mara zote tunawafuata wadau kama nyinyi kusaidia kama mlivyofanya," alisema Bakari Mnondwa. Uboreshaji wa elimu unaofanywa na Serikali kwa kushirikisha wadau kama NMB unasaidia kupunguza kero mbalimbali na kuongeza ufanisi maeneo mbalimbali ya elimu, hivyo kuiomba benki hiyo isichoke kusaidia pale inapoombwa. "..Jamani tunaomba msituchoke nyie ni wadau wetu muhimu hivyo tuendelee kushirikiana," alisisitiza ofisa huyo. Awali akisoma risala kabla ya hafla ya kukabidhiwa msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Karume, Hillgard Lwambusha aliishukuru Benki ya NMB kwa kutambua na kuthamini maendeleo ya elimu Tanzania kwa kile kuisaidia shule hiyo msaada wa vifaa vya kupaulia madarasa mawili jambo ambalo litapunguza changamoto ya upungufu vyumba vya madarasa. "...Ndugu Mkurugenzi Mkuu wa NMB taasisi yako mmeweza kututatulia moja ya changamoto katika kufanikisha kuweka mazingira bora ya utoaji wa elimu bora na sio bora elimu kwa kutoa vifaa ambavyo vitaezeka vyumba viwili vya madarasa," alisema Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Lwambusha.[caption id="attachment_82300" align="alignnone" width="500"]
Shehena ya mbao zilizotolewa na benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kupaulia madarasa mawili vikishushwa katika Shule ya Msingi Karume.[/caption] [caption id="attachment_82303" align="alignnone" width="500"]
Picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa sehemu ya msaada wa mabati, mbao, misumari pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya kupauwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Karume vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. [/caption] [caption id="attachment_82304" align="alignnone" width="500"]
Meneja wa NMB Tawi la Temeke, Christine Lifiga (wa pili kushoto) akimkabidhi Kaimu Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Bakari Mnondwa (wa pili kulia) orodha ya vifaa vya kupaulia madarasa mawili ikiwa ni sehemu ya msaada wa mbao, mabati na misumari pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya kupauwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Karume vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Wengine kulia ni Diwani Kata ya Buza Manispaa ya Temeke, James Raphaeli pamoja na ofisa wa Benki ya NMB (mauzo) Temeke, Rejina Pius [/caption]

No comments