Header Ads

Responsive Ads Here

BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI TANESCO LAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito
Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la
wafanyakazi mjini Tanga

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),
Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa
baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza hilo kulia akiwa na  
Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale wakisikiliza kwa umakini hoja za
wafanyakazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi akizungumza katika mkutano
huo 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi kushoto akifurahia jambo naKaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa Tuico Tanzania,Paul Sangeze akizungumza  katika mkutano huo
Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wajumbe wa baraza
hilo
Mmmoja wa wafanyakazi na mjumbe wa baraza hilo akichangia kwenye mkutano huo
mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Janet Vesso
akichangia mada
Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi wa pili kutoka
kushoto,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito
Mwinuka kulia na 
Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze wa kwanza kushoto niKatibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale
BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
limeazimia kuunga mkono jitihada za Rais  Dkt John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya watu wenye kipato cha kati kwa kufanya kazi kwa umahiri,uzalendo na
ufanisi.

Akizungumza katika ufungaji wa baraza hilo mwishoni mwa wiki
mjini Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi alisema
bodi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha shirika
linafikia malengoyake muhimu.
 
Alisema malengo hayo ambayo yanahitajika katika kuhakikisha
uchumi wa viwanda unafikiwa kwa kasi kubwa kutakapotokana na kuwa na umeme wa uhakika
ambao unaweza kusukuma gurudumu la maendeleo. 
 
 
Aidha alisisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya
shirika hilo ili iweze kusaidia kutoa huduma zake wakati wote bila kuwepo kwa
vikwazo vya namna yoyote ile.

Hata hivyo aliwaasa wafanyakazi wa shirika hilo kuhakikisha
wanakuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili isiweze kuibiwa ikiwemo kuhakikisha
haihujumiwi na watu wanaoweza kufanya hivyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments