Header Ads

Responsive Ads Here

ASSC BINGWA KOMBE LA NYERERE DAY


IMG-20171016-WA0001
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya ASSC A wakiwa na kombe baada ya kukabidhiwa kombe la mashindano ya Nyerere Cup na mwaka mpya wa Kiislamu yaliofanyika juzi jijini hapa Picha na Mahmoud Ahmad -Arusha.
IMG-20171016-WA0003 
Baadhi ya wachezaji wa ASSC A wakisherehekea kwa kupiga picha na vikombe vya ubingwa wao baada ya mashindano ya Nyerere Cup jijini hapa juzi. Picha na Mahmoud Ahmad -Arusha.
………………………………………………………………
Mahmoud Ahmad Arusha
Bonanza la mpira wa miguu kusherehekea Mwaka mpya wa Kiislamu 1439 na kombe la Nyerere 2017 yamefanyika mkoani wa Arusha kwa siku mbili na Kuzishirikisha timu kadhaa kutoka Moshi na wenyeji Arusha katika viwanja ya Kiteck nje kidogo ya jiji la Arusha na ASSC kuibuka bingwa wa mashindano hayo.

Mashindano hayo yalioendeshwa kwa mtindo wa ligi na kuzishirikisha timu sita kutoka mikoa miwili ya Kilimanjaro na Arusha ambapo bingwa wa mashindano hayo alikuwa ASSC A kutoka Arusha ambapo alijizolea Pointi  10  na kupewa zawadi ya kombe kubwa huku ndugu zao ASSC B wakishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 10 lakini wakipitwa kwa uwiano wa magoli waliambulia kombe dogo.
 
Timu ambazo zilishiriki mashindano hayo ni ASSC A na B, Al Fur A na B Al Ikhwa na timu kutoka moshi ambapo mashindano hayo yaliendeshwa kwa mtindo wa ligi hadi kupatikana bingwa
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mtanange huo ambao ulifanyika kwenye viwanja vya Kiteck nje kidogo ya jiji la Arusha mratibu wa mashindano hayo Abdul Rab Hanif  amesma kuwa mashindano hayo huwayanafanyika kila mwaka mpya wa kiislamu unapoanza.
 
Amesema mashindano hayo ya mwaka huu yameenda sambamba na kumuenzi baba wa Taifa hayati Mwalimu nyerere na kuwa Mwalimu alipenda kuona mataifa yote hapa duniani na Afrika yanaishi bila kubaguana kwa misingi ya dini,Kabila wala rangi hivyo ndio maana wameamua kumuenzi kwa michezo.
 
Alifafanua kuwa Baba wa Taifa alikuwa amejipambanua kwa kuwa mtu ambaye hakujikweza ndio maana hata sisi leo hatukubagua watu kwa dini zao wala rangi au kabila kwenye mashindano haya hivyo kila mwaka tutakuwa tukiazimisha mashindano haya kwa kuita timu kutoka dini tofauti na makabila tofauti kuweza kuenzi kwa matendo falsafa ya Mwalimu Nyerere.
 
“Michezo ni Afya na ajira tumekuja kuweka Afya zetu katika hali inayotakiwa na pia kuvumbua vipaji vipya katika mashindano haya ya mpira wa miguu ya kumuenzi baba wa Taifa letu”Alisema Hanif.

No comments