Header Ads

Responsive Ads Here

ASKARI WA JWTZ WAUWAWA NCHINI DRC


1
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  linasikitika kutangaza vifo vya Askari wake wawili Koplo Maselino Paschal Fabusi na Praiveti Venance Moses  Chimboni,  ambao walikuwa katika Ulinzi wa Amani nchini DRC.

Askari hao  wamefariki baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi tukio ambalo limetokea tarehe 09 Octoba 2017 umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni. Majeshi yetu yamefanikiwa kuwarudisha nyuma waasi hao na kudhibiti eneo hilo.
Kufuatia shambulizi hilo Umoja wa Mataifa umeunda Bodi ya Uchunguzi kuchunguza tukio hilo. Aidha, Maafisa na Askari wa JWTZ wanaendelea  kutekeleza majukumu yao katika Operesheni hiyo.
Umoja wa Mataifa unaandaa utaratibu wa kuleta miili ya marehemu nchini.  Mtajulishwa taratibu za mapokezi, kuaga miili ya marehemu hao na mazishi.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi Amina.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
10 Octoba, 2017

No comments