Header Ads

Responsive Ads Here

ASILIMIA 90 YA WAVUVI NCHINI WANATUMIA ZANA DUNI KATIKA SHUGHULI ZAO

WAKATI Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa kitowewo cha samaki kwa siku za karibubi utafiti umeonesha  asilimia 90 ya wavuvi nchini wanatumia zana duni hali inayopelea kuvua samaki tani 52,000 kwa mwaka ambao ni kidogo tofauti na rasilimali zilizopo kwenye bahari ya Hindi.

Hayo yalisemwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi za Maji na Uvuvi,Dk Benaisha Benno alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya uharibifu wa mazingira kwenye bahari uliondaliwa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (WWF).

Benno alisema wavuvi hao hawana vifaa vya kisasa vitakavyowasaidia kuvua samaki katika bahari kuu matokeo yake wanashindwa kuvua samaki wakubwa na wengi ili waweze kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yao.

Alisema sekta ya uvuvi ikitumika kikamilifu itakuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi na wananchi.

"Tafiti ambayo ilifanyika 2014 inaonesha asilimia 90 ya wavuvi wanatumia dhana duni hali ambayo inasababisha washinde kwenda kwenye kina kifupi hivyo wanapata samaki wachache," alisema.

Dk. Benno alisema kutokana na dhana duni wavuvi wameshindwa kuvua katika kina kirefu ambacho ni mita 200 hivyo wanakosa samaki wakubwa kama jodari.

Alisema ni wakati muafaka kwa serikali kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha rasilimali zilizopo baharini zinatumika kwa usahihi.

Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Ta zania(Tafiri),Baraka Kuguru alisema sekta ya uvuvi ikipewa kipaumbele itachangia ukuaji wa uchumi na hivyo kutekeleza malengo ya viwanda na uchumi wa kati.

Kuguru alisema tafiti ziaonyesha kuwa sekta ya uvuvi imekuwa na mchango mkubwa kwa nchi ambazo zimewekeza hasa katika ukanda wa bahari ambapo rasilimali zilizopo kwenye bahari zina thamani ya dola za Marekani 333 bilioni huku uwekezaji ukiwa asilimia 20 mpaka sasa.

Dk.Kuguru alisema pamoja na wavuvi kuwa na vifaa duni vya kuvulia ipo changamoto nyingine ya kuharibu mazalia ya samaki kama matumbao na mikoko hali ambayo inaweza kuchochea uvuaji samaki kupungua.

Alisema pia uwekezaji katika bahari kama kutafuta mafuta na gesi ni shughuli ambazo zinachochea samaki kupotea au kwenda kwenye kina kirefu.

"Bahari kwa sasa inakutana na changamoto nyingi kama uharibifu wa matumbao, kukata mikoko na kutafuta mafuta na gesi hali ambayo inakimbiza samaki katika kina kifupi na kwenda kina kirefu," alisema.

Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja Kampeni ya kulinda Hifadhi ya Selous kutoka WWF, Atilio Tegalile alitoa rai kwa wanahabari kujikita katika habari za mazingira na bahari ili kuweza kusaidia nchi na wananchi hasa wanaojihusisha na uvuvi.

Meneja huyo alisema iwapo kutakuwa na kundi la wanahabari waliojikita kuandika habari za utunzaji mazingira na rasiimali za habari kutakuwa na mabadiliko chanya hivyo dhana ya uchumi wa viwanda itatekeleza kirahisi.

"Natumia nafasi hii kuwaomba mjikite katika uandishi wa aina moja (specialization) kwani ndio uandishi wa sasa na mtapata tuzo, " alisema.

Mmoja wa wavuvi wa soko kuu la samaki la Zanzibar,Hamisi Arafat Hamisi aliiomba serikali iwatengenezee mazingira bora yatakayowawezesha kupata mikopo ili kuweze vitakavyowawezesha kununulia vifaa vya kisasa vitavyoweza kufika bahari kuu ambapo wataweza kuvua samaki aina ya jodari na papa.

Kwa upande wake Mvuvi Omary Hamis alisema changamoto iliyopo ukosefu wa boti yenye uwezo wa kuvuz katika kina kirefu hali inayosababisha kuvua samaki wadogo na wachache.

"Boti tuazotumia zinaweza kuvua mita isiyozidi 30 hivyo kupelekea kupata samaki wachache na wadogo,tunaiomba Serikali isifikilie kuchukua kodi ijikite kwenye uwekezaji wa sekta ya uvuvi kwani ina faida kwa nchi na wananchi,alisema Hamisi.

No comments