Header Ads

Responsive Ads Here

Wizara ya Afya Malawi Yatembelea Muhimbili , Waipongeza Kwa Kutoa Huduma Bora


0001
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Malawi ambao umetembelea hospitali hiyo LEO ili kujifunza jinsi inavyoboresha huduma za afya. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi, Dk. Dan Namarika.

0002
Ujumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru.
0003
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi akieleza muundo wa hospitali kwa ujumbe wa Malawi.
0004 A
Wakurugenzi wa Muhimbili wakiwamo watalaamu wengine wa afya wakimsikiliza Dk Magandi leo.
0005
Ujumbe wa Malawi ikiongozwa na wenyeji wao wakiwa katika Jengo la Watoto leo.  
0006
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na idara hiyo.
0007
Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.
………………………
Dar es salaam                            
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  leo imepokea ujumbe wa wataalamu wa Afya  kutoka Wizara ya Afya ya nchini Malawi.
Ujumbe huo umeongozwa na Katibu wa Afya nchini humo , Dk. Dan Namarika  umehusisha Madaktari , viongozi pamoja na wataalam mbalimbali kutoka katika Wizara hiyo pamoja na taasisi nyingine za afya .
Akizungumza  baada ya kupokea ujumbe huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amesema ujio wa watalaamu hao unatoa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji  katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk.  Juliethi Magandi amesema  katika mwaka wa Fedha  2016-2017  Hospitali  imehudumia wagonjwa  wa  nje Laki Nne , Thelathini na Sita Elfu na Miatatu Tisini na Nne  wakati wagonjwa wa ndani waliohudumiwa ni  Hamsini na Tisa Elfu na Miatano Hamsini na Tano.
Akizungumzia lengo la ujio wao , Katibu wa Afya wa nchi hiyo  Dk. Dan Namarika  amesema wamekuja kujifunza jinsi ambavyo MNH  inafanya kazi  na kutekeleza mipango yake .
Lengo la serikali ya Malawi na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha inaboresha  utoaji wa huduma  hususani  katika Hospitali za Umma nchini humo.
Ujumbe usema kuwa umefurahishwa jinsi Muhimbili inavyotoa huduma za kibingwa na kusomesha wataalamu wa afya nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.

No comments