Header Ads

Responsive Ads Here

WETCU: KIWANDA CHA NYUZI TABORA KIKIONYESHA UWEZO WA KUSAFIRISHA NYUZI HADI KWA MKULIMA TUTAZINUNUA

 

wetcu
Kaimu Meneja wa Manunuzi kutoka Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) Bernard Makhanda (kushoto) akitoa utaratibu wa kufuatwa na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora ili aweze kupata fursa ya kuwauzia nyuzi kwa ajili ya wakulima wa tumbaku. Kulia ni Meneja wa Kanda wa Bodi ya Pamba Jones Bwahama.

rc
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa ufafanuzi jana kwa mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kujionea hali halisi ya uzalishaji wa nyuzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Urveshi Rajani.
picha na RS_Tabora

Na Mwandishi wetu.
RS –TABORA
Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi(WETCU) kisema kuwa kinaweza kununua kamba kutoka Kiwanda cha Nyuzi Tabora kama watakuwa tayari kuzisambaza hadi kwenye Vyama vya Misingi(AMCOS) na kwa bei nafuu isiyowauza wakulima.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Meneja wa Ugavi wa WETCU Bernard  Makhanda jana mjini Tabora wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali wanaotumia bidhaa za pamba na wamiliki wa Kiwanda hicho ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa WETCU inaunga mkono juhudi za Serikali za kuinua viwanda vya ndani kwa kununua bidhaa zilizozalishwa hapa nchini na kufikisha huduma karibu na wakulima wa tumbaku.

Makhanda alisema kuwa baada ya kupitia maombi ya Kampuni na watu mbalimbali waliomba kusambaza kamba ,wanachosubiri ni kukutana na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora kwa ajili ya kujadiliana jinsi ambavyo wanaweza kufikisha bidhaa hizo kwa wakulima kupitiaa Vyama vyao vya Msingi(AMCOS) badala ya kuishia kwa WETCU.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono Kiwanda hicho kwa kununua bidhaa mbalimbali wanazozalisha kwa ajili ya kukiwezesha  kuongeza uzalishaji na kutoa ajira kwa watu wengi na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali.
Aliongeza kuwa wamiliki wa Kiwanda hicho wamesema wanaweza kuongeza uzalishaji wa nyuzi kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama kama watakuwa na uhakika wa soko.
Naye Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Urveshi Rajani alisema kuwa yuko tayari kuzalishaji nyuzi nyingi iwapo viwanda vya nguo hapa na Chama Kikuu cha Ushirika wa wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) wakimuunga mkono katika kuchukua bidhaa zake.
Alisema kuwa Kiwanda hicho kilipunguza uzalishaji kwa sababu ya Viwanda vya hapa nchini vilivyokuwa vinachukua nyuzi kwake kwa ajili ya kutengenezea nguo kuanza kuagiza bidhaa hizo kutoka nje ya nchi na hivyo yeye kukosa soko.
Naye Mkuu wa Wilaya Tabora Queen Mlozi alisema kuwa wapo wakulima wa tumbaku ambao alikutana nao na kumhakikishia kuwa kamba zinazozalishwa na Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora ni bora sana.
Kufuatia hali aliwaomba wamiliki wa Kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa kamba kwa kuwa soko lipo kubwa kwa wakulima wa tumbaku.
Kiwanda cha Nyuzi Tabora hivi sasa kinao watumishi 24 badala ya 350 waliokuwepo hapo awali.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora yupo katika ziara ya kukagua viwanda mbalimbali kuangalia hali halisi ya uzalishaji wake kama vipo ambavyo vimeshindwa viweze kuchukuliwa kwa ajili ya kuwapa wawekezaji wengine.

No comments