Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI MWAKYEMBE, PAUL MAKONDA WAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MUHINGO RWEYEMAMU VIWANJA VYA MNAZI MMOJA


01
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Harisson Mwakyembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda wakiongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza la Mwili wa Marehemu Muhingo Rweyemamu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo, Marehemu Muhingo Rweyemamu ambaye aliwahi kuwa Mwandishi wa Habari Nguli enzi za uhai wake na Mkuu wa Wilaya kadhaa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania alifariki juzi  na anazikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Professor Faustin Kamuzora.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
1
Picha mbalimbali zikionyesha Jeneza la Mwili wa Marehemu Muhingo Rweyemamu ukiwasili kwenye kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam tayari kwa shughuli za waombolezaji kutoa heshima za mwisho leo.
234
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe wakitoa heshima za mwisho katika jeneza la Mwili wa Marehemu Muhingo Rweyemamu.
56
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Professor Faustin Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mh. Kanali Ngemela Lubinga wakitoa heshima zao.
7
Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Wilaya jijini Dar es salaam wakiongozwa na Edward Mpogolo Katibu Tawala Wilaya ya Ilala wakitoa heshima zao.
8
KATIBU Tawala wa wilaya ya Kigamboni Ndg Rahel Mhando akiongozana na baadhi ya viongozi kutoa heshima za mwisho kushoto ni aliyekuwa  Mkuu wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela.
9
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar Bw. Salum Mwalimu pamoja na Mh. Jaquline Liana kushoto wakitoa heshima zao.
10
Athman Khamis akimpa pole Mke wa Marehemu mara baada ya kutoa heshima zake.
11
Teddy Mwapunda kulia na Barda Masoud wakitoa heshima zao;
12
Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media Bw. Tido Muhando na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Francis Nanai nao wakijumuika na waombolezaji kutoa heshima zao.
13
Mtaalam wa  Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN Tanzania) Bi. Hoyce Temu na Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Bw. Bakari Machumu wakitoa heshi za zao za Mwisho kushoto ni Mkurugenzi Sehemu ya Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus.
14
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Harisson Mwakyembe akizungumza na Mtaalam wa  Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN Tanzania) Bi. Hoyce Temu  na Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Montage.
15
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda akizungumza na Mdau Athman Khamis.
16
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na Bw. Albert Kilala Mtangazaji wa kituo cha Chanel Ten.
17
Waombolezaji Salva Rweyemamu kulia na Juma Pinto wakijadili jambo katika msiba huo.
1819
Jeneza lenye mwili wa marehemu Muhingo Rweyemamu.
20
Picha mbalimbali zikionyesha waombolezaji waliofika kutoka heshima zao za mwishi kwa mwili wa marehemu Muhingo Rweyemamu.
2123

No comments