Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI LUKUVI ATOA MSAADA WA AMBULANCE JIMBONI KWAKE


Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi na mbunge wa jimbo la ismani Williamu Lukuvi akiwa kwenye gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser alilokabidhi kwa halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini ambalo ni rafiki na mazingira kwa tarafa ya pawaga mkoani Iringa.

Waziri
wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi na mbunge wa jimbo la ismani Williamu Lukuvi akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza sambamba na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakitafakari jambo wakati wakukabidhi gari la wagonjwa kwa viongizi wa halmashuri ya wilaya ya Iringa vijijini
Huu ndio muonekano wa gari la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa na waziri Lukuvi kwa ajili ya mahitaji ya kituo cha afya cha Idodi
 
Na Fredy Mgunda,Iringa.
 
Waziri
wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi na mbunge wa jimbo la ismani Williamu Lukuvi
ameendelea kuboresha sekta ya afya katika tarafa ya idodi kwa kuwapa gari la
kisasa la kubebea wagonjwa linaloendana na mazingira ya tarafa hivyo kwa ajili
ya matumizi ya kituo cha afya cha Idodi.

Gari hilo aina ya Toyota Land
Cruiser lilikabidhiwa kwa uongozi wa halmashauri ya Iringa vijijini
inayosimamia uendeshaji wa kituo cha afya cha Idodi katika mkutano mkubwa wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha Idodi tarafa ya Idodi.
Akikabidhi msaada huo Lukuvi
alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na familia ya
Karimjee Jivanjee kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa tarafa ya Idodi na hiyo
yote imetokana na uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya
tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Ismani.”

Alisema gari hilo la wagonjwa
ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza
kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.

Baada ya kukabidhi gari hilo, lukuvi
ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake
kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha jimbo hilo linapata huduma bora ya
maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.
MH Lukuvi aliwataka wananchi na
viongozi kulitunza gari hilo ili litumike kwa muda mrefu kwa wamanufaa ya wagonjwa.

“Jamani gari hili ni rafiki na
mazingira yetu hivyo naombeni tulitunze hili gari kadri tuwezavyo maana magari
ya kubebea wagonjwa ni gharama kubwa sana hivyo ni lazima tuwe na uchungu wa
vitu tunavyopewa kwa msaada”alisema Lukuvi

Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa iringa Amina Masenza alimshukuru waziri Lukuvi kwa
kijihada anazozifanya kuboresha sekta ya afya katika jimbo la Ismani
.
“Tuna wabunge wengi hapa
nchi ila ni wabunge wachache sana ambao wanaokumbuka wananchi wao hivyo
niendelee kumpongeza mheshimiwa waziri kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta
maendeleo katika jimbo la Ismani na Iringa kwa ujumla” alisema Masenza

Akishukuru kwa msaada huo, Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Iringa vijijini, Stephen Mhapa alisema kabla ya msaada huo, kituo
hicho cha afya kilikuwa kina gari moja ambalo nalo lilikuwa limeharibia
kutokana na kutokuwa na mazingira rafiki na barabara za tarafa hiyo.

Alisema kupatikana kwa gari hilo
jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo kwa kuokoa maisha ya wagonjwa na maisha
ya mama na mtoto ambayo ni kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.
Naye diwani wa kata ya Idodi Onesmo
Mtatifikolo alisema atahakikisha inatekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na
Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk John Magufuli, mbunge na madiwani ili
kuboresha huduma ya afya wananchi wa tarafa ya Idodi.
Nao baadhi ya wanachi wa
tarafa ya Idodi walimpongeza waziri Lukuvi kwa msaada wa gari la wagonjwa
pamoja na kuanza kutatua tatizo la wafugaji na wakulima kwa vitendo

No comments