Header Ads

Responsive Ads Here

WATUMISHI WANAOTOA HUDUMA KWA VIONGOZI KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KULETA MABADILIKO YA UFANISI ZANZIBAR

Na Kijakazi Abdalla    Maelezo        
Katibu Mkuu  Wizara ya Nchi,Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salim Maulid Salim amewataka watumishi wanaotoa huduma kwa viongozi kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko ya ufanisi katika shughuli zao.

Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Wizara ya Habari , Utamaduni ,Utalii na Michezo wakati akifunga mafunzo ya mapishi na ukarimu kwa wafanyakazi ambayo yameendeshwa na Wakufunzi  kutoka katika Taasisi ya China National Research Institute of Food and Fermentation Industries.
Alisema kuwa kufanyakazi kwa bidii kutaweza kuwapa mabadiliko katika kazi zao na kuwajengea uwezo katika kutoa huduma bora na kuwacha kufanya kazi kwa mazoea
Aidha Katibu huyo alisema mafunzo hayo yamewezesha watumishi hao  kujenga ushirikiano na  mahusiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China na kuendelea kuwa na uhusiano wa kidugu na wa kihistoria pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha amewashukuru wakufunzi  kwa kuwapatia watumishi hao mafunzo ambayo yatawawezesha kuwapa maarifa mapya na utaalamu ili  kumudu kutekeleza majukumu  kwa ufanisi zaidi.
Nao Wahitimu wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuwapatia mafunzo hayo jambo ambalo litawezesha kubadilika katika kazi zao na kuweza kujielewa.

No comments