Header Ads

Responsive Ads Here

WANANCHI WAITIKIA WITO WA SERIKALI WA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA


7357
Baadhi ya wananchi wakiwa katika chumba cha usajili tayari  kusajiliwa.

7346
Hawa ni baadhi tu ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la Usajil Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa. Kwa sasa zoezi hili linafanyika kwa awamu ngazi ya Kata ili kutoa fursa kwa wananchi wote wenye sifa kusajiliwa.
7336
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akiingiza taarifa za wananchi kwenye mfumo kabla ya kuchukua taarifa za kibaiolojia za wananchi wa Kilolo ambako zoezi kwa sasa linaendelea.
7334
Mmoja wa wananchi akichukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kukamilisha hatua za Usajili Vitambumnbulisho vya Taifa. Mkoa wa Iringa ni moja ya Wilaya zinazo endelea na Usajili kwa sasa kati ya mikoa 11 ya Tanzania.
…………………………
Wananchi wa Wilaya ya Kilolo wameendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa baada ya kukamilisha awamu ya kwanza ya usajili ambayo ni kujaza fomu za maombi ya Usajili na fomu zao kupitishwa na Serikali za Vijiji wanakoishi.
Zoezi linaenda sambamba na uhakiki wa taarifa za wananchi wanaoomba kupewa vitambulisho vya Taifa chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya Mitaa na Vijiji kabla ya kutoa nafasi kwa wananchi  kuweka  Mapingamizi ya wazi kwa wale waombaji wanaotiliwa shaka uraia wao kabla ya kuendelea na mchakato wa Uzalishaji.
Wilaya ya Kilolo ni Wilaya ya mwisho kukamilisha zoezi hili kwa mkoa wa Iringa na hivyo kutoa fursa ya kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho vya Taifa kielektroniki.
Mbali na Iringa mikoa mingine inayoendelea na zoezi hilo ni ya Kanda ya Ziwa ikiwemo; Geita, Shinyanga, Mwanza, Manyara na Singida.

No comments