Header Ads

Responsive Ads Here

WANAFUNZI WALIOPATA AJALI YA KUZAMA KWENYE MAJI WILAYA YA GEITA WAKABIDHIWA MTUMBWI WA INJILI KWA AJILI YA KWENDA SHULE


Mtumbwi wa Injini  ambao umekabidhiwa kwenye visiwa vya Butwa na Rulegea kwaajili ya kusafirisha wanafunzi ukielekea kwenye makabidhiano.


Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo wa chama Tawala cha CCM pamoja na wanafunzi Akizungumza kwenye shule ya Msingi ya Butwa wakati wa makabidhiano.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ,Mhandisi Modest Aporinali Akielezea Juu ya ushirikiano ambao wanao kati ya Halmashauri hizo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,Wilaya ya Geita Barnnabas Mapande akielezea juu ya ilani ya chama hicho katika kutekeleza ahadi ambazo wanatoa kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Geita,Ali Kidwaka akisoma taarifa ya  utekelezaji wa ahadi ambayo wameitoa kwenye vijiji hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikabidhi Mtumbwi huo wa kisasa kwa mwenyekiti wa Rulegea na Butwa.
Serikali
Mkoani Geita imekabidhi Mtumbwi wa Injini kwenye Kisiwa cha Rulegea Kijiji cha
Butwa, mtumbwi wenye thamani ya Sh Milioni 7 kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
wanaolazimika kuvuka maji kwenda shuleni.
Mtumbwi huo
wa kisasa umekabidhiwa kutokana na tukio la kuzama kwa wanafunzi waliokuwa
wakitoka shuleni June 22 mwaka huu na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu.
Akikabidhi
mtumbwi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezekiel Kyunga, Mkuu
wa wilaya ya Geita Bw Herman Kapufi amemtaka mwenyekiti wa kijiji Butwa Bw
Mashauri James na wananchi kuweka mchango wa mafuta ya mtumbwi huo.
“Nakukabidhi
Mtumbwi huu na vifaa vyake vyote ni jukumu lenu kuutunza na kuhakikisha watoto
wanakwenda shule kila siku na isije kutokea mtoto kutokwenda shule naamini
kwamba mtautunza na utawafaa zaidi wanafunzi”Alisisitiza Kapufi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw Ali Kidwaka amesema Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanikisha upatikanaji wa
usafiri huo.
Akishukuru
kwa niaba ya wananchi  mwenyekiti wa
kijiji Butwa Bw Mashauri James amemwakikishia Mkuu wa Wilaya kuutunza vizuri
mtumbwi huo na kwamba wataweka utaratibu
upatikanaji wa mafuta.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

No comments