Header Ads

Responsive Ads Here

Wanafunzi 14 wa vyuo vikuu nchini katika kinyang’anyiro cha Global Management Training ya ABINBEV

Student tbl 1
Meneja vipaji wa TBL Group na ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Lilian Makau (kulia) akiwa na baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa katika awamu ya kwanza ya mchujo wa kuingia  mafunzo ya utawala wa kibiashara ya ABINBEV.(Kushoto) ni Meneja wa Programu hiyo ya mafunzo,eth Baise.

student tbl 2
Wanafunzi walioingia kinyanganyiro cha  awamu ya kwanza wakijieleza
student tbl 3
Wanafunzi walioingia kinyanganyiro cha  awamu ya kwanza wakijieleza
student tbl 4student tbl 5student tbl 6
Baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa wakisikiliza maelezo wakati wa  usahili.
student tbl 7
Afisa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi akitoa ufafanuzi wakati wa usahili huo
student tbl 8
Baadhi ya wanafunzi wasichana waliofuzu kuingia mchujo wa awamu ya kwanza wakiwa kwenye chumba cha usahili
student tbl 9
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group  na ABINBEV wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu walioshiriki kwenye usahili.
………………………………………………………………
Awamu ya kwanza ya mchakato wa kuwapata wanafunzi wa vyuo vikuu walioomba kujiunga na mafunzo ya kimataifa ya uongozi wa kibiashara (Global Management Training Program) ambayo yalizinduliwa hivi karibuni nchini na kampuni mama ya TBL Group ya ABINBEV nchini unaendelea ambapo katika awamu ya kwanza wanafunzi 14 kutoka vyuo vikuu mbalimbali wamefuzu kuingia katika mchujo wa awamu ya kwanza na usahili  kwa wanafunzi hao ulifanyika mwishoni mwa wiki katika  hoteli ya SeaCliff jijini Dar es Salaam.
Akiongea juu ya program hiyo,Mkurugenzi wa  masuala ya sheria na masuala ya nje wa TBL na  ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Georgia Mutagahywa,alisema kuwa inafurahisha kuona  maelfu ya vijana wamejitokeza kuomba  kuingia kwenye program hiyo japo nafasi sio nyingi ambapo baada ya kuyapitia maombi wamechaguliwa wanafunzi 14 na mchakato wa kuwafanyia usahili unaendelea ili kupata 3   watakaoungana na wenzao kutoka nchi mbalimbali za Afrika kupata mafunzo hayo ya kuwaandaa kuwa viongozi wa biashara na viwanda baada ya miaka michache ijayo.
TBL na ABINBEV tunafurahi kuona vijana wa kitanzania wanapata fursa hii ya kuwapatia utaalamu wa kuongoza biashara na uendeshaji wa shughuli za viwanda kwa ufanisi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania ina mkakati mkubwa wa kuimarisha sekta ya viwanda nchini.Programu hii ni endelevu tuna imani itawanufaisha vijana wengi wa kitanzania”Alisema Mutagahywa.
Kwa upande wake,Meneja wa Kuendeleza vipaji wa ABINBEV kanda ya Afrika,Rene Kohler-Thomas,alisema kuwa  mafunzo haya yameishaonyesha mafanikio makubwa katika nchi ambazo kampuni hiyo inaendesha  biashara zake na sasa  ndio yamezinduliwa rasmi  barani Afrika.
Alisema katika kipindi cha awamu ya kwanza ya mafunzo haya zimechaguliwa nchi za Afrika ya Kusini,Tanzania,Kenya na Nigeria na lengo kubwa ni kuwanoa vijana wahitimu wasio na uzoefu wa kazi kupata elimu na uzoefu na wakishahitimu kupatiwa fursa za uongozi wa  ngazi za juu katika biashara za kampuni zilizopo kwenye nchi mbalimbali.
“Ndoto yetu kubwa kama kampuni ni kuwaleta watu pamoja katika ulimwengu maridhawa (Better World) katika kutimiza ndoto hii na kuhakikisha bidhaa zetu zinaingia katika  masoko mapya moja  ya mkakati wake ni  kuvutia wateja wapya na kuondoa mipaka na ndio maana tunatoa fursa kwa wote kujiunga na kufanya kazi na sisi”.Alisema Rene Kohler-Thomas
Alisissitiza kuwa hii ni fursa pekee kwa vijana wa kitanzania watakaochaguliwa kujiunga na program hii inayojulikana kama Global Management Training Programme kwa kuwa watapata ujuzi wa fani mbalimbali sambamba kupata mafunzo ya vitendo kwenye kampuni zilizopo chini ya ABINBEV sehemu mbalimbali duniani.
   Rene Kohler-Thomas   alisema   kwa watakaofanikiwa  kujiunga watapata mafunzo kwa muda wa miezi 10 mfululizo ambapo wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo ndani na nje ya kampuni kwenye nchi mbalimbali na kukutanishwa na kuzungumza na wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali za uendeshaji wa biashara na utawala.
“Wahitimu walengwa zaidi katika program hii ni waliohitimu katika fani za Biashara,Uchumi,Masoko,Uhasibu na fedha,Uhandisi na IT na fani nyinginezo wenye vipaji kwa kuwa kampuni yetu inaamini katika kuwekeza katika  viongozi wa baadaye na ndio maana tumekuja na mpango wa kuwaandaa”.Alisema.
Mmoja wa wanafunzi waliofuzu kuingia kinyanganyiro cha awamu ya kwanza, Ajra Omary,kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi,akiongea kwa niaba  ya wenzake alipongeza jitihada hizi na kuongeza kusema kuwa uwekezaji unaolenga kuleta manufaa kwa jamii ndio unaotakiwa kwa kuwa unafungua milango ya  ajira kwa watanzania na kuwapatia fursa za uongozi wazawa  baada ya kupatiwa mafunzo ya kitaalamu hususani katika kipindi hiki kuelekea Tanzania ya viwanda

No comments