Header Ads

Responsive Ads Here

Walemavu Waiomba Serikali Kuwakumbuka na Changamoto za Elimu Bure


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wenyeulemavu ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenyeulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Doris Kulanga akizungumza kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.


Mjumbe wa SHIVYAWATA, Nasiria Ally (kulia) akichangia mada leo kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. Kushoto ni mtafsiri wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi akizungumza leo kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. Kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Mikono, Maimuna Kanyamela.

WATU wenye ulemavu wameiomba Serikali kuwatazama katika jicho la pekee katika fursa iliyopo ya utekelezaji wa sera ya elimu bure inayotekelezwa kwa wananchi wote kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne. Wakizungumza leo katika mjadala wa wazi kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017
linaloendelea jijini Dar es Salaam, wamebainisha watoto toka familia za watu wenye ulemavu baadhi
wanashindwa kufaidi fursa hiyo kutokana na umbali zilipo shule za msingi na sekondari huku familia zao
zikishindwa kugharamia usafiri kwa watoto hao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wenyeulemavu ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenyeulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Doris Kulanga ametoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mjadala, huku akiziomba taasisi anuai na Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.
Alikubali kuwa kundi la wanawake lina changamoto zinazowakabilia lakini kundi la wanawake walemavu
wanachangamoto kubwa zaidi kutokana na kukabiliana na vikwanzo mbalimbali vya uchumi na hata huduma
za kijamii ikiwemo elimu. “Ukiangalia elimu kwa sasa ni bure toka darasa la kwanza hadi sekondari, lakini
watoto toka familia za watu wenye ulemavu tunashindwa kufaidi fursa hii kutokana na shule hizo kuwa na
umbali nasi kushindwa kugharamia nauli kwa watoto wetu,” alisema Bi. Kulwanga ambaye ni mlemavu asiyeona.
Alisema familia nyingi za watu wenye ulemavu zinakipato duni hivyo kushindwa kugharamia nauli kwa watoto wao kutokana na umbali zilipo shule na makazi hivyo kuiomba Serikali na wadau wengine kuangalia namna ya kuzisaidia familia hizo kukabiliana na changamoto hiyo.
Naye Mjumbe wa SHIVYAWATA, Nasiria Ally ambaye ni kiziwi alisema kundi hilo limetelekezwa kielimu ukilinganisha na makundi mengine. Alisema shule za viziwi nyingi hazina vifaa vya kutosha na hata ukiangalia kwenye vyombo vya maamuzi hawashirikishwi. Alisema kundi hilo linashindwa kuingia hata katika ushindani wa siasa kutokana na kutokuwa na mazingira ya kuvutia katika kushirikishwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi alishauri wadau wa masuala ya
maendeleo kuangalia usawa wa elimu na nyanja zingine za fursa zinaifikia jamii yote bila vikwanzo ili kila mmoja aweze kunufaika na fursa zilizopo.
Bi. Liundi alisema bado changamoto ya umbali wa shule za sekondari na ukosefu wa mabweni kwa shule hizo unawaathiri zaidi watoto wa kike kwa kujikuta wanaingia kwenye lindi la mimba za utotoni hasa katika familia za hali ya chini (kipato duni) tofauti na ilivyo kwa wamilia zenye uwezo.
Alisema suala hili la changamoto likiachwa Tanzania itajikuta inaingia katika uchumi wa viwanda huku ikitelekeza makundi ya jamii, jambo ambalo zitawalazimu kushindwa kunufaika na fursa hiyo ya maendeleo ya kiuchumi. “Tuingie katika uchumi wa viwanda huku makundi yote ya kijamii yakinufaika na fursa hiyo na si kuachwa nyuma,” alisema Mkurugenzi, Bi. Liundi.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) Merry Lusimbi akizungumza leo kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.

Sehemu ya washiriki kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.

Mkurugenzi wa taasisi ya Mikono Yetu, Maimuna Kanyawela akizungumza leo kwenye mjadala wa wazi katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. Kulia ni Anna Mwasha Mkurugenzi Idara ya Kuondoa Umasikini Wizara ya Fedha na Uchumi.

Baadhi ya wanafunzi wakishiriki kwenye mjadala wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.

No comments