Header Ads

Responsive Ads Here

WAKULIMA WASHAURIWA KUTUMIA MBEGU BORA KUONGEZA UZALISHAJI


2.
Wakulima wa zao la Maharage Mkoani Songwe wakiandaa maharage kabla ya kuyahifadhi katika magunia tayari kwa mauzo na usafirishaji katika maeneo mbalimbali.Na Mwandishi Wetu,
Songwe

WAKULIMA wa zao la maharage Mkoani Songwe wameshauri utumia vyema fursa ya mafunzo kutoka Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) kupitia mradi wa uhakika wa mbegu kwa chakula na kipato ili kuweza kuongeza tija ya uzalishaji na kipato katika kaya.

Hayo yamesemwa hivi karibuni Wilayani Momba na Mkuu wa Idara ya Kilimo toka shirika la Action for Development Program (ADP) Mathius Lisso ambaye pia ni bwana shamba wa mradi wa  uhakika wa mbegu kwa chakula na kipato unaotelekezwa na shirika la PELUM Tanzania kupitia ufadhili wa Taasisi ya Bread for the World.
Lisso amesema kupitia mradi huo wakulima katika vikundi hivyo watawezesha mbegu hizo kutumiwa na wakulima wengine nje ya vikundi hivyo kwa kuwa mbegu zimekidhi ubora unaotakiwa kwa mujibu TOSCI.
 “Wakulima hawa kwa sasa mbali na kufanikiwa kuandaa mbegu zao wenyewe kupitia wataalamu toka TOSCI l pia jamii inayowazunguka wameanza kunufaika na uwepo wa mbegu hizi baada ya kuona uzalishaji wake uko tofauti kulinganisha na mbegu za asili” amesema Lisso.
Ameongeza kuwa ambapo kupitia mbegu hizo mkulima atakuwa na uwezo wa kupata gunia sita hadi nane kwa heka moja iwapo atazingatia  kanuni, ikilinganisha na mbegu za asili ambapo kwa kwa ekari moja mkulima ana uwezo wa kupata debe tatu hadi  tano pekee.
Lisso amesema mbegu ambazo wakulima hao wanazozalisha ni aina ya Njano Uyole na Uyole 96 ambazo maharage yake yana soko kubwa katika nchi ya DRC Kongo na Tunduma na hivyo kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo ambayo imeanza kuleta matokeo chanya kwa wakulima kupitia uzalishaji wake.
Aidha Lisso amelipongeza shirika la PELUM Tanzania kwa kutambua mchango wa wakulima wadogo katika kukuza sekta ya kilimo na kutafuta fursa za miradi mbalimbali na kupanua wigo wa ushirikiano Maafisa kilimo na ugani wa Serikali.
Kwa mujibu wa Lisso amasema miongoni mwa malengo ya mradi huo ni kuunganisha mtandao wa wakulima nchini kupitia vikundi hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji hivyo ni wajibu wa TOSCI kutoa utambulisho wa vyeti kwa wakulima walio kwenye vikundi ili waweze kuwafundisha wakulima.
Kwa upande wake, mmoja wa wanakikundi cha Motomoto Erasto Mauli mmoja wa amesema mbali na mbegu hizo kuanza kutumiwa na wakulima wenzao ndani ya kata pia wameweza kupanua wigo wa masoko hadi maeneo ya Tunduma.
Mauli alisema uwepo wa mizani feki kutoka kwa umesababisha wengi wao kutopata faida hali inayochangia mkulima kunyonywa, kwani mbali na dalali kupata faida ya shilingi 5000-7000 kwa kila debe bado anakuwa na faida ya kilo tatu hadi nne kwa kila debe kutokana na madebe yao kuwa makubwa.
Mradi wa uhakika wa mbegu kwa uhakika wa chakula na kipato unaofadhiliwa na wa Bread for the World na kusimamiwa na Shirika la PELUM Tanzania na kutekelezwa katika ya Mikoa Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Kigoma, Songwe, Mbeya, Manyara na Shinyanga.

No comments