Header Ads

Responsive Ads Here

“Wakandarasi tumieni vyombo vya habari kutangaza kazi zenu ili mpate soko kwa urahisi”.Prof.Elisante


01
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasiliasha mada kuhusu Ubunifu,Masoko na Ujasiliamali  wakati wa mkutano Mkuu wa Bodi ya Wakandarasi (ERB)  Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion Center jana Mjini Dodoma.

02
Wajumbe wa Mkutano wa mkuu wa Bodi ya Wakandarasi (ERB) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Ubunifu,Masoko na Ujasuliamali  katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion Center leo Mjini Dodoma. Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.
………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-WHUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Wakandarasi nchini kutumia vyombo vya habari katika kutangaza ufanisi na ubunifu wanaoufanya ili kupata soko kwa urahisi.
Prof. Elisante ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha mada ya kuhusu Ubunifu, Masoko na Ujasiriamali katika mkutano Mkuu wa Bodi ya  Wakandarasi  nchini ambao hufanyika mara moja kila mwaka.
“Wakandarasi ni watu muhimu sana katika jamii yetu maana wamekuwa wakituvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, maji na mawasiliano. Hivyo, ni muhimu kwenu kushirikiana na vyombo vya habari katika kueleza mafanikio hayo” amesema Prof. Elisante
Prof. Elisante aliongeza kuwa vyombo vya habari ni njia rahisi na ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa jamii katika kile kinachofanywa na watu wake hivyo ni budi wahandisi kufanya kazi na waandishi wa habari katika kueleza yale waliyofanikisha.
Aidha, Prof. Elisante amewataka wakandarasi hao kutumia fursa ya ujasiriamali, ubunifu na masoko katika kuhakikisha bidhaa zao zinapata soko na kuuzwa kwa wingi ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujmla.

No comments