Header Ads

Responsive Ads Here

WADAU WA MICHEZO JITOKEZENI KUDHAMINI MCHEZO WA WUSHU; MHE.ANNASTAZIA


PIX 1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa mashindano ya nne ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yaliyomalizika jana Jijini Dar es Salaam yaliyojumuisha nchi za Tanzania na Rwanda.

PIX 2
Mwakilishi wa Ubalozi wa China  hapa nchini Gao Wei akizungumza  katika hafla ya kufunga wa mashindano ya nne ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yaliyomalizika jana Jijini Dar es Salaam yaliyojumuisha nchi za Tanzania na Rwanda. Wa kwanza kushoto ni  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura.
PIX 3
Baadhi ya Wachezaji wakicheza mmoja wa mchezo wa WUSHU katika Hafla ya kufunga mashindano ya nne ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yaliyomalizika jana Jijini Dar es Salaam yaliyojumuisha nchi za Tanzania na Rwanda.
PIX 4
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akimvisha medali ya ushindi mmoja wa washindi wa mchezo wa WUSHU baada ya  wa mashindano ya nne ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yaliyomalizika jana Jijini Dar es Salaam yaliyojumuisha nchi za Tanzania na Rwanda.
………………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Katika uhakikisha mchezo wa WUSHU unakuwa na kutengeneza ajira kwa watu wengi  hapa nchini Serikali imeomba wadau kudhamini na   kuwekeza  katika mchezo  huo ili ufahamike kwa kuwa Serikali tayari meandaa mazingira ya kupata wataalamu wa kufundisha mchezo huo.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam  na Naibu  Waziri  wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Annastazia Wambura alipokuwa akifunga mashindano ya nne ya kimataifa ya mchezo huo ambapo amesema Serikali tayari imeanza kutengeneza mazingira ya kupata wataalamu wa kufundisha mchezo huo kupitia chuo cha michezo Malya.
“Tumeshasaini  Mkataba na Serikali ya China kwa ajili ya kutupatia wataalamu wa kufundisha mchezo huu katika chuo chetu cha michezo  Malya, tunaamini wataalamu hawa watasaidia kukuza mchezo huo hapa nchini” Alisema Mhe.Annastazia.
Aidha amewataka wachezaji wote wanaocheza mchezo huo kucheza kwa malengo ya kufanikiwa  lakini pia kutangaza nchi yetu ndani na nje ya nchi  kupitia mchezo huo  ambao unaendelea kukua kwa kasi hapa nchini.
Kwa upande wake mwakilishi wa Ubalozi wa China  hapa  nchini  Gao Wei ameishukuru Serikali  ya Tanzania kwa ushirikiano walionao na China katika kufanikisha mchezo huo hapa nchini na kuahidi kutoa wataalamu wengi wa kufundisha WUSHU ili kuwapatia vijana wengi ajira.
“Mchezo huu unasaidia sana kuimarisha ushirikiano wetu wa muda mrefu kama tunavyoshirikiana katika masuala ya Utamaduni na Sanaa” Aliongeza Gao Wei.
Washiriki wa mcheo huo wameelezea kunufaika na mchezo huo ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kwenda kujifunza zaidi mchezo huo nchini China na kuahidi kurejea  kuwa mabalozi wazuri wa kufundisha mchezo huo.
Mchezo wa WUSHU ni mchezo unaojumisha michezo mingi ikiwemo Judo na Ngumi na kwa hapa nchini unachezwa katika mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Tanga  Lindi na Mtwara ambapo mashindano ya mwaka huu  yamejumisha nchi ya Rwanda, China na Wenyeji Tanzania na yamemalizika jana.

No comments