Header Ads

Responsive Ads Here

WADAU WA ELIMU WA NDANI NA NJE NCHINI WAKUTANA DODOMA KUJIONEA MAFANIKIO,CHANGAMOTO PAMOJA NA KUBORESHA SEKTA YA ELUMI HIYO


1Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akifungua Mkutano wa pamoja wa wadau wa elimu waliokutana mjini Dodoma leo, ili kufanya mapitio ya sekta ya Elimu.

2Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda akitoa salamu za Wizara wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa Elimu mjini Dodoma.
3
Wadau wa elimu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano
4
Wadau wa elimu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano
………………………………
Wadau wa Elimu wa ndani na nje ya Nchi leo wamekutana mjini Dodoma kwa lengo la kufanya mapitio ya sekta ya elimu ili kujionea mafanikio, changamoto na kutafuta njia za pamoja za kutatua changamoto hizo kwa maslahi mapana ya kuboresha Sekta ya elimu nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, SayansinaTeknolojiaDkt. Leonard Akwilapo amesema mkutano huo una lengo la kujadili utekelezaji wa mipango ya elimu ya mwaka uliopita, kutathmini na kuweka mipango ya pamoja ili kutekeleza malengo yaliyowekwa katika sekta ya elimu.
Alisema Mkutano huo utawawezesha wadau wa elimu kupata fursa ya kupitia utekelezaji wa shughuli mbalimbali na kuwasilisha changamoto walizokutana nazo wakati wa utekelezaji na kwa pamoja kutafuta namna gani wanaweza kupata ufumbuzi wa pamoja ili kuboresha upatikanaji wa elimu.
Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Elimu kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Tixon Nzunda amesema “Sisi kama watekelezaji wa Sera, Viwango na miongozo inayotolewa na Wizara ya Elimu tunatumia jukwaa hili kuwasiliana na wadau kuhusu namna bora ya kuondoa vikwazo vinavyoweza kupunguza kasi ya kuwawezesha watoto kupata Elimu bora”.
Aliongez akuwa kwa pamoja tutaweka mipango ya kuhakikisha tuna jenga miundo mbinu ya shule, tunaboresha mazingira ya kufundishia, kuimarisha taaluma ya Elimu bora ili kuweza kutoa Elimu bora kwa watoto wote na kutomuacha mtoto yeyote Nje ya Mfumo.
Mkutano huu wa siku nneu natarajiwa kuhitimishwa Alhamisi Septemba 21, 2017.

No comments