Header Ads

Responsive Ads Here

VITENDO VYA KISHIRIKINA KANDA YA ZIWA VINASABABISHA MAUAJI KWA WATU WASIO NA HATIA


MIKOA KANDA YA ZIWA

Na Tiganya Vincent-Nzega
Wakazi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kishirikina na kuwa na hofu ya Mungu na hivyo kuachana na mauaji ya watu mbalimbali wakiwemo wazee wenye macho mekundu, wakinamama wanaohisiwa kuwa wachawi na watu wenye ulemavu.


Kauli hiyo imetolewa jana na Mmiliki wa Studio ya Big D Entertainment na Mlezi wa Kwaya ya Watoto wa Kanisa la African Inland Church(T) la Nzega mjini John Dotto wakati wa uzinduzi wa Kanda ya Nyimbo za Mchungani Egon Israel yenye kubeba jina la Nakuombea Jirani.

Alisema kuwa watu wanaomcha Mungu na walioshika maagizo yake hawezi kuwaua wazee kwa sababu ya kuonekana kuwa na macho mekundu yaliyotokana na uzee wao na wala hawezi kufirikia kuwaua wenye ulemavu wa ngozi .
Doto alisema njia pekee ya kuondokana na aibu hiyo hasa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa ni kuhimiza watu wote kwa imani zao katika maeneo hayo kuishi misingi ya dini yake na maelekezo ya Mungu yanayotolewa na viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, Masheikh na Makasisi.
Alisema kuwa inapotekea jambo lolote sio zuri katika maeneo hayo kama vile ugonjwa na kifo baadhi ya wenyeji wamekuwa wakimbilia katika kuamini kuwa wamerogwa na kuanza kuwasihi watu na kuchukua hatua ambazo sio sahihi.

Katika kuhakikisha kuwa neno la Mungu linawafikia watu wengi kwa njia ya nyimbo Doto aliahidi kuwa tayari kuwazisaidia bure Kwaya zote za Kanisa hilo ambazo zitahitaji kurekodi katika Studio yake nyimbo zinazotoa ujumbe wa neno la Mungu kama sehemu ya kuhamasisha jamii kumcha Mungu na kuachana na aibu ya kila mara mikoa ya kanda ya ziwa kunyoshewa vidole kwa ajili ya mauji yanakuwa yamechangia kuamini ushirikina.

Doto alisema kuwa pesa wanazitumia na nguvu wanazozitumia kuondoa maisha ya watu wasio na hatia zitatoa ushahidi mbele ya Mungu siku ya hukumu na kuwaomba watu kutumia nguvu zao na akili walizojaliwa kutafuta mali kwa njia halali.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Regina Athuman alisema kuwa jina la wimbo uliobeba mkanda la Nakuombe jirani linawataka Watanzania kuishi kwa upendo na ushirikino.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwafanya kuachana na vitendo viovu na vinavyosababisha baadhi yao kushawishika na kwenda kuwatendea maovu wazee na watu wenye ulemavu.

Akisoma risala wakati wa uzinduzi wa albunu hiyo Katibu wa Kanisa la AICT –Nzega  Walwa  Milambo kwa niaba ya mchungano Egon Israel alisema kuwa uzinduzi huo unalenga kupanua huduma ya kiroho ikiwemo kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na ununuzi wa vifaa vya kurekodia nyimbo.

Alisema kuwa lengo ni kutaka watu wengi wapate neno la Mungu kwa njia ya maubiri na nyingi ili waweze kuondokana na matendo maovu na yanayorudisha nyuma maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Katika uzinduzi huo wa albamu ya Ninakuombea Jirani Mmimiliki wa Studio ya Big D Entertainment John Doto alitoa milioni 1 na wadau wengine walichangia shilingi milioni 1.5 ambapo jumla ilikuwa milioni 2.5.

Mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita na Mwanza  imekuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo watu wenye ulemavu wa ngozi na wazee wakuwa wakiripotiwa kutendewa unyama ikiwemo kuwawa.

No comments