Header Ads

Responsive Ads Here

VITAMBULISHO VYA TAIFA VYABISHA HODI MKOA WA NJOMBE


2017-09-22 at 1208
 kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe wakifuatilia kwa Karibu yale yaliyokuwa yakizungumzwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendela wakati huu Mkoani humo pamoja na Wilaya zake zote.

2017-09-22 at 1203
Wakiwa kwenye Picha ya Pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa njombe Mh. Christopher Ole Sendeka, Wakuu wa Wilaya za Njombe, kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe, Afisa Usajili Mkoa wa Njombe Ndugu. Odoyo Godwin Albetus pamoja na Paroko wa KKKT jimbo la Njombe.
2017-09-22 at 1206
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Christopher Ole Sendeka akihutubia Viongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na Wageni waalikwa katika shughuli ya Uzinduzi wa Zoezi la Usajili na Utambuzi Mkoani Njombe.
2017-09-22 at 1205
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Ndugu Ali Kasinge ambae alimuwakilisha Mwenyeji wa Uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Lucy Msafiri, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa na wageni waalikwa katika Uzinduzi wa Usajili na Utambuzi wa Vitambulisho vya Taifa lililofanyika Njombe Mijini.
2017-09-22 at 1204
Afisa Usajili Mkoa wa Njombe Ndugu. Odoyo Godfrey Albetus akisoma Taarifa fupi ya zoezi la Usajili pamoja na Mpango kazi utaotumika kukamilisha zoezi hilo na kufikia Malengo tarajiwa ya Kusajili Wananchi 426,083 katika Mkoa huo wa Njombe.
2017-09-22 at 1207
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Zaina Mlawa akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi Mkoani Njombe.
…………….
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka amezindua rasmi kuanza kwa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa huo, zoezi ambalo linaendeshwa katika Wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Ludewa, Njombe Mjini, Makete pamoja na Wanging’ombe.
Akizungumza katika sherehe fupi ya uzinduzi wa zoezi hilo kimkoa Mhe. Ole Sendeka amewataka Wakuu Wote wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa, Watendaji Kata na Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa/Vijiji kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kufanishika zoezi hilo Msingi ili kutimiza malengo ya Serikali ya Kuwasajili Wananchi wake wote ifikapo Desemba 2018.
Amesema manufaa ya Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ni mengi na hasa upatikanaji wa huduma kirahisi na kuimarisha ulinzi na Usalama wa nchi.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Wakuu wote wa Wilaya, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa za Mkoa wa Njombe, Viongozi wa dini na wananchi.
Zoezi la Usajili katika Mkoa wa Njombe litahusisha uchukuaji na ujazaji wa fomu za maombi ya Vitambulisho, uchukuaji wa alama za Kibaiologia, saini ya kielektroniki, kupigwa picha na zoezi la uhakiki na mapingamizi litakalohusisha Kamati za Ulinzi na usalama na wananchi.  Mkoa huo unategemea kusajili jumla ya Wananchi 426,083 kwa kipindi cha Miezi 2 kwa mpango maalumu ambao utahusisha usajili wa Mkupuo (Mass-Registration).

No comments