Header Ads

Responsive Ads Here

VIDEO:MSUVA AING’ARISHA DIFAA EL JADIDI KUIBUKA NA USHINDI WA KWANZA DHIDI YA RAPIDE OUED ZEM LIGI YA MOROCCO


Screenshot_20170731-014900-660x400
Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Mabingwa watetezi wa Vodacom Tanzania bara,Simon Msuva ameisaidia timu yake ya Difaa Hassani El Jadidi kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Rapide 0ued Zem Mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco ijulikanayo kwa jina la Botola Pro uliochezwa kwenye dimba la Stade El Abdi Mjini El Jadidi.

Jadidi ulikuwa mchezo wao wa pili wa Ligi baada ya kuanza kwa sare hatimaye wamezinduka na kupata ushindi wa kwanza wa Msimu kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa timu zote mbili kwani ziliweza kushambuliana huku zikicheza kwa kasi.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko na katika dakika ya 66 wageni Rapide 0ued Zem walikuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa na Imad Errahouil baada ya kupiga chenga mabeki wa Jadidi na kuwashangaza wenyeji hata hivyo Ayoub Nanah alisawazisha dakika ya 71.
Kuingia kwa goli hilo Jadidi waliliandama lango la wageni kama nyuki huku Msuva akifanya kazi kutoa pasi na katika dakika ya 89 Hamid Ahaddad alifunga goli la pili kwa wenyeji kwa njia ya mkwaju wa Penalti baada ya beki wa Rapide kucheza rafu ndani ya boksi na dakika ya 90 Chouaib El Maftoul alipigilia msumari wa tatu.
Hadi mwamuzi anamaliza Mpira Difaa Hassani El Jadidi wameibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Rapide 0ued Zem kwa Matokeo hayo Jadidi wamefikisha jumla ya pointi nne na kushika nafasi ya tano wakiwa wamecheza mechi mbili na Septemba 30 watakuwa ugenini kucheza na Wydad Casablanca

No comments