Header Ads

Responsive Ads Here

UMOJA WA WAZEE WAKULIMA KONGOWE (UWAKO)WALILIA MAFUNGU YANAYOTOLEWA KWA AJILI YA WAZEE


IMG-20170928-WA0027

IMG-20170928-WA0029
Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha
UMOJA wa wazee wakulima kata ya Kongowe ,wilayani Kibaha ,Mkoani Pwani (UWAKO),unasikitishwa kukosa mafungu ya wazee ambayo hutolewa kwa ajili ya kuwasaidia .
Aidha umoja huo umewataka wataalamu wa kilimo kujenga tabia ya kukaa na wakulima na kuwaelimisha kilimo cha kisasa pasipo kukaa na utaalamu wao kwenye vitabu na maofisini .
Akizungumzia matatizo yanayowakabali wazee hao ,wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali alivyowapatia mtafiti wa mazingira na misitu kutoka -TAFORI- Ibrahim Mkwiru ,mwanzilishi wa umoja huo ,mzee Mrisho Mfyome (Nigogogo),alisema hawapati misaada wala mafungu yanayopaswa kupewa wazee.
Alieleza wazee wa Kongowe wamekuwa wakisikia kwenye bomba manufaa na haki hizo kwa wenzao kwenye maeneo na mikoa mingine pekee.
Mzee Mfyome ,aliomba serikali kuanzia ngazi za chini ,wilaya na mkoa kuwatupia macho ili nao wanufaike kama wazee wengine .
Hata hivyo ,alieleza wanakabiliwa na changamoto ya elimu haba ya kilimo na kukosa hati miliki ya maeneo yao ili kujiendeleza na kilimo chenye tija .
“Wataalamu wa kilimo ,watoke maofisini nao watafute vyama na umoja unaojishughulisha na masuala ya kilimo ili kuweza kuwasaidia kuinua sekta ya kilimo na kuwapa ujuzi wa kisasa katika sekta hiyo ” alisema mzee Mfyome.
Nae katibu wa UWAKO ,Yusuph Chuma (Lule),alisema kwasasa wana shamba lenye hekari 100 huko Ruvu ,linalowasaidia kujikomboa kimaisha .
Kati ya hekari hizo 50 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na 50 kwa lengo la ufugaji nyuki ambapo wameweka mizinga zaidi ya 30 ya nyuki .
Chuma alisema ,mwaka 2013 walijiunga wazee wenye nia na dhamira moja ya kujiinua kiuchumi ili kujitoa kwenye wimbi la utegemezi .
Alifafanua kwasasa UWAKO ina jumla ya wanachama 60 wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea .
Mdau wa masuala ya mazingira na misitu ,mtafiti kutoka TAFORI ,Mkwiru aliwapongeza wazee hao kwa kujiunga kwani kuwa mzee haimaanishi kushindwa kujiendeleza wenyewe ama kuwa tegemezi ndani ya familia .
Aliukabidhi umoja huo,mizinga 30 ya nyuki ,majembe ,mapanga ,lake ,mashine ya kumwagilia na vifuko vya kuoteshea miche ya miti 10,000,vyote hivyo vikiwa vimegharimu sh.mil tatu .
Mkwiru aliwaomba wadau wengine wa mazingira na kilimo kuguswa kusaidia wazee hao na makundi yanayojishughulisha na kilimo ili kukamilisha ndoto zao .
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya vifaa hivyo ,ambae pia ni mlezi wa UWAKO ,Edwin Shunda aliuchangia umoja huo sh.100,000 kwa ajili ya kununua majembe ,na kuahidi kuwanunulia t-shirts za chama hicho 20 .
Aliutaka umoja huo ushikane na usirudi nyuma .
Shunda alisema fursa kwa makundi maalum ni nyingi ikiwemo kundi la wazee hivyo atahakikisha anasimamia matatizo yao katika ngazi husika .
Mlezi huyo wa UWAKO, Shunda mapema wiki hii alichaguliwa pia kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM)Kibaha Mjini .

No comments