Header Ads

Responsive Ads Here

UKOSEFU WA USHAIDI KIKWAZO CHA KUKABILINA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO


3
Washiriki wa kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam wakifuatilia jambo wakati salamu za ufunguzi wa kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.

4
Washiriki wa kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam wakifuatilia jambo wakati salamu za ufunguzi wa kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
5
Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Margaret Mussai akifungua kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam.
6
Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Watoto katika Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto UNICEF Bi. Maud Droogleever Fortuym akitoa salamu kutoka UNICEF wakati kikao kazi cha Siku moja na wawakilishi kutoka Shirika La Watoto Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam.
……………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma
Matokeo ya utafiti wa vichocheo vya ukatili dhidi ya watoto yanaonesha bado  matendo ukatili dhidi ya watoto yamekuwa yakiongezeka kila siku hapa Nchini kutokana na wanajamii kufanya matendo hayo bila kujua kama yana athari kwa watoto hao.
 Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Margaret Mussai amesema hayo wakati wa kikao kazi cha Siku moja na wawakailishi kutoka Shirika La Watoto Duniani UNICEF na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti wa vichecheo vya ukatili dhidi ya Watoto leo jijini Dar salaam.
Bi. Margret Mussai amesema utafiti huu ni mwendelezo wa utafiti wa awali wa mwaka 2009 uliotafiti kuhusu ni namna gani mila na desturi zetu zinachangia ukatili kwa watoto hapa Nchini ambapo matokeo ya utafiti huo ndiyo yalisababisha kufanyika utafiti mya juu ya vichocheo vya ukatili dhidi ya watoto.
Mkurugenzi huyo amewataka Wazazi na awalezi hapa Nchini kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kuondoa uoga unaowafanya watoto wao kushindwa kufanya mawasiliano ya karibu na wazazi kwani ukatili dhidi ya watoto katika ngazi ya familia umekuwa ukifanywa na watu wakaribu au jamaa wa wanafamilia.
Aidha Bi. Margret amesema kuwa kariabu na mtoto, kumpenda na kumtunza mtoto hujisikia kupendwa, kuwa salama na  hivyo kujenga uwezo kujiamini na kumweka huru kuzungumza na wazazi wake akisema kuwa mtoto anachukua mengi kutoka kwenye jamii uku juhudi bibafsi kutoka kwenye familia kupotea kutokana na wazazi kuwa mbali na watoto wao.
Bi. Margret pia amekemea tabia ya baadhi ya Wananchi kukataa kutoa ushahidi mahakamani pale makosa ya ukatili yanapowasilishwa mahakamani kwasababu watu wanofanyia watoto ukatili ni watu walio karibu yao hivyo kitendo cha wananchi kushindwa kutoa ushaidi kinakwamisha juhudi za serikali kupambana vitendo vya ukatili ukizingatia kuwa haki haiwezi kutendeka bila kuwepo na ushahidi wa kutosha.
Aidha amezitaja juhudi za serikali katika kupambana na ukatili dhidi ya watoto kuwa nikuweko kwa sheria ya mtoto, kuwepo kwa mkakati wa kitaifa wa  kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na uwepo dawati la mtoto katika vituo vyote vya polisi hapa Nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Watoto katika Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto UNICEF Bi. Maud Droogleever Fortuym amesema, utafiti wa vichocheo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto umefanywa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Huddersfield cha uingereza na umefanyika baada ya matokeo ya awali ya utafiti wa mwaka 2009 yaliyoongalia ni jinsi gani mila na desturi zilizopo katika jamii zinachangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Alibainisha kuwa, katika utafiti huo njia zinazoangaliwa ni zile za ukatili ukiwepo ule wa kimwili, kiakili, kutojaliwa kwa watoto pamoja na unyanyasaji na mpango wa kwanza wa utafiti ulikuwa wa miaka mitano na ulianza 2013-2016 na sasa wako katika mpango wa pili 2016-2021.

No comments