Header Ads

Responsive Ads Here

UFUNGUZI WA UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO WAFANYIKA ZANZIBAR


DSC_0675
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia  akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa  Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

DSC_0713
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa  Maradhi ya Kinywa na Meno  katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
DSC_0728
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika  Zoezi la Uchunguzi wa  Maradhi ya Kinywa na Meno  katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
DSC_0773
Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt,Ismail Amour akitoa Elimu ya kujikinga na maradhi hayo katika  Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa  Maradhi ya Kinywa na Meno  katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
DSC_0800
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kushoto akifanya mahojiano na Muandishi wa Habari kutoka ITV Farouk Kariym pamoja na  muandishi wa Habari Maelezo Zanzibar Khadija Khamis katika  Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa  Maradhi ya Kinywa na Meno  katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
DSC_0836
Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Haspitali ya Arrahma Zanzibar akimfanyia Uchunguzi wa  mardhi ya Kinywa na Meno Kauthar Vuai mkaazi wa meli nne, katika Zoezi la Uchunguzi wa  Maradhi ya Kinywa na Meno  katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
………………………………………………………………………………….
Na  Khadija Khamis –Maelezo
Jamii inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya  ikiwemo  afya ya kinywa na meno ili  kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi  ya afya angalau mara mbili kwa mwaka .
Hayo aliyaeleza na  Mkurugenzi  wa Kinga na Elimu ya Afya  Dr  Fadhil Mo’hd Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa afya ya  kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .
Alisema afya  hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa ushauri  wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza meno .
Alifahamisha kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa  elimu kwa wanafunzi pamoja na kung’oa meno kwa  wale ambao meno yao yameadhirika .
Aidha alisema mpango huo wa uimarishaji  afya ya jamii iko haja kurejea utaratibu  wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na vijijini .
“Huu usiwe  mwanzo  wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.
Alieleza kutoa  elimu na uchunguzi wa afya  kwa jamii itasaidia kupunguza gharama za matibabu  na kuimarisha  kinga ya awali na kujiepusha na matumizi ya vyakula  ambavyo vinachangia kuleta madhara ikiwemo vyakula vya sukari  kuchangia  uozeshaji wa  meno hasa kwa watoto .
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno ( TBA) Dr Lorna  Carneiro  alisema mara hii wamepata fursa ya kuja Zanzibar kwa kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ili kujua wale wagonjwa  ambao wanamatatizo na  kuwapatia tiba pamoja  na kuwapa  elimu ya afya .
Alisema Chama hicho  kinahimiza umuhimu  wa afya bora kwa jamii na kutoa ushauri  wa maradhi mbalimbali ikiwemo ukimwi ,saratani ,Kifua kikuu,afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza  kwa kuifanya jamii ipate uelewa  na kujikinga na maradhi ambayo yanauwezo wa kuepukika .
“Hali ya idadi ya  Wagonjwa ni kubwa wakati ya kuwa  magonjwa  haya yanakingika  kwa haraka na kupona lakini kikwazo ni kuwa na uchache wa madaktari ,“alisema Dr Lorna .
Alifahamisha kila ifikapo tarehe 20  machi ya kila mwaka huadhimisha siku ya afya ya kinywa na meno kwa mwaka ujao wanatarajia uzinduzi  wa zoezi hilo litafanyika  Zanzibar .
Nae Mgonjwa BI Nargisi Uzia ambae alifika kupatiwa huduma ya matibabu katika kituo hicho  alisema anaishukuru Serikali kwa kuwaletea wataalamu wa kuchunguza afya zao lakini pia iko haja ya zoezi hilo liwe endelevu kwani  matatizo yako mengi yanahitaji uchunguzi.

No comments