Header Ads

Responsive Ads Here

TUWASA KUNUNUA TENKI LA KUSAIDIA UMWAGILIAJI WA MICHE YA MITI MKOANI TABORA


Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Tabora (TUWASA)imeamua kutoa tenki la kuhifadhia maji ambayo yatatumika kwenye umwagiliaji miche ya miti katika vitalu vya Kitete ili kukabiliana na upungufu wa maji kwa ajili ya shughuli hiyo .

Kauli hiyo imetolewa jana mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa (TUWASA) Mkama Bwire wakati akijibu ombi la Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipotembelea vitalu vya miche ya miti vya Manispaa ya Tabora na vile vya Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mkoa wa Tabora ya upandaji miti ambapo hivi sasa inaendelea na maandalizi ya miche za miti katika maeneo mbalimbali itakayopandwa wakati wa masika.
“Sisi kama Mamlaka ya Maji Safi tunaunga mkono juhudi zako Mkuu wa Mkoa na kwa kutambua juhudi zako …na kwa kutambua hilo tutanunua  tenki kubwa la kuhifadhia maji na kuliweka katika kitalo hiki ili watumishi wanaohusika na usimamizi wa mbegu hizi wasipate shida ya maji wakati huu wa kiangazi” alisema Bwire
Alisema kuwa watalijengea sehemu ya kuliweka katika chanzo cha maji katika eneo la Kitete na kuweka pampu kwa ajili ya kuvuta maji kutoka kisimani na kwenda katika tenki hilo ili wahusika wachukue kutoka hapo.
Afisa Mistu Manispaa Caroline Steven Kyaruzi alisema kuwa tatizo la ukame limesababisha upungufu wa maji kiasi kupata shida wakati wa umwagiliaji kwa sababu eneo linalotumika kuhifadhi maji ni dogo na linachukua maji machache.
Alisema kuwa ili kuondokana na tatizo hilo ni vema wakapata tenki kubwa ambalo watalitumia kuhifadhi maji.
Caroline alisema kuwa kwa sababu ya kukosa tenki kubwa la kuhifadhia maji wanapata shida pindi magari ya Kampuni zinazojenga barabara yanapokuja kuchukua maji wanajikuta wakiwasubiri wamalize kuchota wao ndio nao waanze.

No comments