Header Ads

Responsive Ads Here

Tumieni Fursa za Utafiti wa Madini na Mafunzo Kupitia AMGC- Prof. Mdoe

Pic 1
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja ya Mkutano wa MakatibU Wakuu kutoka Nchi Wanachama wa Kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC). Wengine katika picha ni wawakilishi kutoka Nchi wanachama pamoja Makamishna na Wakuu wa Vituo vya Madini.

Pic 2
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati) baada ya kufugua kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Nchi Wanachama wakiwa katika Kituo cha Afrika Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC). Wengine ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kushoto) na Assa Mwakilembe (kulia).
Pic 3
Baadhi ya wawakilishi wa Bodi ya Kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC), wa kwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UNECA, Dkt. Koja Busia, Mwenyekiti wa Bodi, Masresha Gebreselassie, Mwenyekiti wa AUC, Frank Mugyenyi na Mkurugenzi Mkuu wa AMGC, Ibrahim Shaddad.
Pic 4
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (anayeongea). Wengine ni washiriki katika kikao hicho.
Pic 5
Mshauri Mwelekezi wa AMGC, Timo Gawronski akitoa maelezo kwa washiriki wa kikao wakiwa  katika maabara ya uchunguzi wa asili  ya madini husika.
………………………………………………………………….
Jonas Kamaleki- MAELEZO
Watanzania wametakiwa kutumia fursa zinazopatikana katika kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC) ikiwemo kutumia maabara za kisasa za uchunguzi wa madini.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe wakati wa kikao cha makatibu wakuu, makamishina wa Madini wa nchi wanachama wa kituo hicho.
“Wanafunzi wa vyuo vikuu wameanza kutumia kituo hiki katika masomo yao kitu ambacho ni faida ya uwepo wa kituo hicho muhimu barani Afrika,hapa nchini,”alisema Prof. Mdoe.
Prof. Mdoe amezitaja kazi za kituo hicho kuwa ni kufanya utafiti na kuongeza thamani ya madini, kutoa mafunzo na ushauri wa masuala ya madini na kuhifadhi na kusambaza taarifa za madini zinazohusu nchi wanachama na kuweka kanzidata ya madini.
Licha ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka arobaini tangu uanzishwaji wa AMGC zipo changamoto ambazo zinakikabili kituo hicho kama Prof. Mdoe alivyoainisha kuwa kutolipa michango ya uanachama kwa wakati, jambo ambalo linazorotesha utendaji wa kazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa AMGC, Ibrahim Shaddad amezitaka nchi za kiafrika ambazo hazijajiunga, kujiunga ili kupata manufaa ambayo yanapatikana kwenye kituo hicho.
Aidha, Shaddad amesema Kituo kimeanza kutafuta namna ya kujiendesha ili kuepukana na kutegemea michango ya wanachama ambayo haikidhi haja na matakwa ya AMGC.
Amewahamisisha nchi wanachama kutumia maabara za kisasa zilizopo kituoni hapo na huduma nyingine kama vile mafunzo na ushauri ili kupata manufaa yatokanayo na kituo hicho.
Kituo hiki ambacho ni cha kipekee barani Afrika kwenye utafiti na uchunguzi wa Madini mwaka huu kinatimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake. Kwa sasa kina jumla ya nchi wanachama nane zikiwemo, Angola, Kenya, Burundi, Uganda, Sudan, Ethiopia, Msumbiji na wenyeji Tanzania.

No comments