Header Ads

Responsive Ads Here

TFF YAWATAJA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MECHI YA AZAM FC DHIDI YA SIMBA JUMAMOSI UWANJA WA CHAMAZI


azam-vs-simba_nsvtm3ugt43k191l1ftwpdoo4
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewatangaza waamuzi watakaochezesha mechi kati ya Azam FC dhidi ya Simba, Jumamosi.

Waamuzi haoni Ludovic Charles wa Tabora ambaye atasaidiana na Ferdinand Chacha (Mwanza) Abdallah Mkomwa (Pwani) na Josephat Bulali atakayekuwa mezani.

Tayari mechi hiyo imekuwa gumzo, hii ni kutokana na Simba kuanza ligi kwa kazi kubwa  kutokana na Azam FC kuwa imeamua kufanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuwaacha nyota wake zaidi ya watano.

Timu zote zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mechi za kwanza za Ufunguzi kushinda Simba walipata ushindi wa magoli 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting huku Emmanuel Okwi akifunga magoli manne na Matajiri wa jiji la Dar Azam FC walipata ushindi ugenini wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji timu ya Ndanda FC.

No comments