Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Kuendelea Kufanikisha Elimu ya Ufundi Kwa Vijana wa kitanzania


TBL AWARD DODOMA 2
Waziri Mkuu ,Mh.Kassim Majaliwa akikabidhi cheti kwa Mwakilishi wa TBL Group, Emmanuel Christopher (kushoto),kutokana na mchango unaotolewa na kampuni kukuza elimu ya ufundi nchini,(katikati ) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama
MARIAM 1
Mariam Zayumba mmoja wa wahitimu kupitia program hiyo akichapa kazi katika kiwanda cha TBL Mwanza
KURWA 1
Kulwa Kwangu mmoja wa wahitimu wa programu hiyo akiwa mitamboni katika kiwanda cha TBL
…………………..
 
  KAMPUNI ya TBL Group imeeleza kuwa itaendelea kuunga mkono jitihaza za serikali kupunguza ajira nchini  kwa kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata elimu ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA kupitia mpango maalumu wa kupata elimu zaidi ya vitendo kuliko nadharia unaojulikana kitaalamu kama Dual Apprenticeship programme
 
Akihojiwa mjini Dodoma muda mfupi baada ya kupokea cheti cha kutambua mchango wa kampuni kuendeleza vijana kupitia elimu ya ufundi  wakati wa hafla ya  uzinduzi  wa miongozo ya Kitaifa ya Kusimamia Mafunzo ya Vitendo kwa  Wahitimu (Internship Guidelines) na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Guidelines) mahala pa kazi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Kassim Majaliwa,Mwakilishi wa TBL Group,Emmanuel Christopher,alisema kampuni inaamini kuwa mpango wa kuwapatia vijana elimu ya ufundi utawezesha kupunguza tatizo la ajira nchini na ndio maana ni mdau wake.
 
Alisema vijana   waliofadhiliwa na kampuni hiyo na kupatiwa mafunzo katika fani ya umeme wa viwandani kupitia program hiyo wameweza kupata maarifa makubwa ya kazi kwa vitendo kwenye kiwanda cha TBL cha Ilala ambapo baada ya kuhitimu masomo  wameweza kuajiriwa na wanaendelea kufanya vizuri.
“Mpango huu utasaidia kuodoa tatizo la ajira nchini hususani katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchumi wa viwanda kwa kuwa viwanda ni moja ya sekta yenye nafasi nyingi za ajira na vinahitaji wataalamu wa fani mbalimbali hususani zile za ufundi”.Alisema Christopher.
 
Wakati wa kuzindua miongozo hiyo,Waziri Mkuu,Mh.Kassim Majaliwa alisema itasaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi yenye weledi wa kutosheleza mahitaji ya soko la ajira na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

No comments