Header Ads

Responsive Ads Here

TBL Group kuadhimisha Global Beer Responsible Day 2017


Kuhamasisha zaidi unywaji kistaarabu kwa jamii
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBEv mwishoni mwa wiki hii itaadhimisha siku ya Unywaji wa kistaarabu ambayo huadhimishwa Septemba 15 kila mwaka kwa kushiriki kampeni mbalimbali zinazowahamasisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na viwanda vya kampuni hiyo kuvitumia  vizuri kwa ajili ya kuwaletea burudani na kuimarisha afya zao na sio kuwaletea madhara wao binafsi na kuleta athari kwa jamii.
Akiongea katika mahojiano maalumu kuhusiana na maadhimisho hayo yanayojulikana kama Global Beer ResponsibleDay (GBRD),Meneja  wa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi,alisema japo  kampuni mama ya ABInBev  na TBL Group imeanza kutekeleza mkakati wa  kuhamasisha unywaji wa kistaarabu kwa jamii kwa muda mrefu lakini imetenga siku maalumu katika mwaka kwa lengo la kuwekea msisitizo suala hili kwenye  maeneo  yote duniani inakoendeshea biashara zake.
Katika siku ya Global Beer Responsible kwa upande wa Tanzania ambayo itafanyika siku ya Jumamosi ijayo wafanyakazi wa TBL Group nchini watashiriki kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusiana na unywaji wa kistaarabu kwa makundi mbalimbali ya jamii ambapo pia watagawa vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya vinywaji kwa ustaarabu”.Alisema.
Mutiganzi alisema  kwa lengo la kufanikisha  malengo yaliyokusudiwa katika kampeni hii inawahusisha wadau mbalimbali kwenye jamii sambamba na  wadau wanaoshirikiana kibiashara na kampuni  wengi wao wakiwa ni wasambazaji wa vinywaji,wamiliki wa mabaa,wafanyakazi kwenye mabaa na watumiaji wa vinywaji kwa ujumla.
Mutiganzi aliongeza kusema kuwa TBL Group kwa muda mrefu imekuwa ikiendesha kampeni za unywaji wa kistaarabu ambazo zimekuwa zikienda sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza  changamoto ya ajali nchini.”Tumekuwa na kampeni kubwa ya kuhamasisha madereva kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa,semina mbalimbali kuhusu madhara ya ulevi kwa makundi mbalimbali,kutoa elimu ya unywaji wa kistaarabu kwa wadau wetu katika biashara,kuweka nembo kwenye bidhaa zetu kuhusiana na kutowauzia vinywaji vyenye kilevi watoto wenye umri mdogo usioruhusiwa kutumia vinywaji”.Alisema.
Hatua nyingine za kuhamasisha unywaji wa kistaarabu ambazo kampuni imefanikisha alizitaja kuwa ni kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya ndani kuhusu madhara ya utumiaji mbaya wa vinywaji vyenye kilevi ambapo hawaruhusiwi kuingia katika maeneo ya kazi wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi,kuzingatia kanuni za utangazaji wa bidhaa za kampuni zenye kilevi,kushiriki semina na makongamano ya kampeni na kuongelea unywaji wa kistaarabu,
 
Alisema  suala la kuhamasisha unywaji kistaarabu liko katika sera ya kampuni ya ‘’Dunia Maridhawa” ambayo inahamasisha kujenga jamii yenye  afya bora sambamba na utunzaji wa mazingira. “Tutaendelea kuadhimisha siku hii  kwa vitendo ambayo ilizinduliwa na ABInBev mnamo mwaka 2010 na tunawakaribisha  wadau wote kushirikiana nasi katika kampeni za kuhamasisha unywaji wa kistaarabu na kutuunga mkono kwa kuzingatia matumizi  mazuri ya vinywaji vyetu ili kufanikisha lengo lililokusudiwa ikiwemo ufanikishaji wa malengo Endelevu ya Millenia (SDGs) ’’.Alisema.

No comments