Header Ads

Responsive Ads Here

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YASHEREHEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI ‘YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA AFYA NA KUGAWA DAWA BURE KWA WANANCHI’

 

Siku ya Moyo 1
 Afisa Lishe wa  Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Louiza Shem akitoa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya moyo wakati wa  Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Taasisi hiyo. Pamoja na kutoa elimu ya afya bora Taasisi hiyo imetoa huduma ya upimaji afya bila malipo na kutoa dawa bila malipo kwa kushirikiana na makampuni yanayotengeneza dawa za binadamu na Shirikisho la Magonjwa yasiyo kuwa ya Kuambukiza (TANCDA).

Siku ya Moyo 2
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Mary Haule akimpima sukari Charlote Guzuye mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam wakati wa  maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Siku ya Moyo 3
Waandishi wa Habari wa kituo cha Televisheni cha Tumaini wakifanya mahojiano na bibi Lena Mwambija mkazi wa Kinyerezi jijini Dar Es Salaam aliyefika katika viwanja vya   Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo bila malipo ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani.
Siku ya Moyo 4
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lucy Nyawike akimpima shinikizo la damu  (BP) Mwandishi wa Habari wa kituo cha  Televisheni cha Clouds Rachel Chizoza wakati wa  maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Siku ya Moyo 5
Daktari Bingwa wa Magonjwa  ya Moyo  kutoka Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aloyce Mohamed akimkabidhi dawa za ugonjwa wa moyo Abdala Shomvi  mkazi wa Mkuranga Mkoani Pwani wakati wa  maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Siku ya Moyo 6
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lucia Kabeya akimpima msukumo wa damu  (BP) Subir wakati wa  maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Siku ya Moyo 7
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania Bwahama akimpima sukari Shabani Juma  wakati wa  maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni ya dawa na chama  ilitoa  upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Siku ya Moyo 9
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji  magonjwa ya moyo bure  wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
Siku ya Moyo 10
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Lugendo akimpima shinikizo la damu (BP) Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa Leyla Faiz wakati wa  maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo na kutoa dawa bila malipo kwa kushirikiana na makampuni yanayotengeneza dawa za binadamu na Shirikisho la Magonjwa yasiyo kuwa ya Kuambukiza (TANCDA). 
Picha na Paschael  Dotto – Maelezo

No comments