Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA MUHIMU KWA WANANCHI KUHUSU USAJILI WA WAZEE WA WILAYA YA UBUNGO VITAMBULISHO VYA TAIFA


nida_clip
USAJILI WA WAZEE WA WILAYA YA UBUNGO VITAMBULISHO VYA TAIFA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inapenda kuwajulisha wazee wote wa mkoa wa Dar-es-salaam Wilaya ya Ubungo kuwa, zoezi la Usajili na Utambuzi lenye lengo la kuwapatia Vitambulisho vya Taifa linaendelea sambamba na zoezi la Usajili wa Kadi za Bima ya Afya kwa wazee chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Wahusika ni wazee wote wanaoishi Wilaya ya Ubungo. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua na kujaza fomu ya maombi ya  Usajili. Fomu zinapatikana ofisi ya Mtaa unakoishi au Ofisi ya Kata. Unapojaza fomu ya maombi unatakiwa kuweka na nakala ya  viambatisho muhimu vinavyokutambulisha vile ulivyonavyo mathalani Kadi ya Kupigia kura, Barua ya Serikali ya Mtaa, vyeti vya shule na kisha fika na fomu yako ikiwa imejazwa pamoja na vivuli (photocopy) ya viambatisho hivyo kwenye kituo cha karibu kusajiliwa.
Unapofika kusajiliwa unashauriwa kwa ajili ya ubora wa picha kutovaa nguo nyeupe, kijivu, bluu, pinki, au rangi yoyote inayoshabihiana na nyeupe, nguo zenye nembo, kofia aina yeyote ama kupaka hina kwenye viganja vya mikononi.
Kwa kuanza wiki ijayo Ratiba ya Usajili itakuwa ni kama ifuatavyo:-
NaKITUO CHA USAJILIMUDATAREHE
1.Kata ya  Makurumla

Saa 3:00 – 11:00 jioni11/09/2017
2.Kata ya Manzese

Saa 3:00 – 11:00 jioni12/09/2017
3.Kata ya SinzaSaa 3:00 – 11:00 jioni13/09/2017
4.Kata ya MakuburiSaa 3:00 – 11:00 jioni14/09/2017
 Utaratibu wa Usajili katika Kata zingine tutaendelea kuwafahamisha. Kupata maelezo zaidi tafadhali wasiliana na mtendaji wako wa Mtaa au Mtendaji Kata.
 Kwa taarifa zaidi kuhusu Vitambulisho vya Taifa tembelea Tovuti yetu www.nida.go.tz au ukurasa wetu wa facebook -nidatanzania au twitter @nidatanzania
 Wazee jitokezeni kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa ili mtambulike na kupata huduma za kijamii kwa haraka na kwa uhakika zaidi.
 Limetolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

No comments