Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 25.09.2017

  • MTOTO MCHANGA AMEOKOTWA AKIWA AMETUPWA CHOONI WILAYANI ILEMELA.


  • MTU MMOJA ANATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA KUMPIGA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA BAADAE KUJINYONGA HADI KUFA WILAYANI MISUNGWI.
KWAMBA TAREHE 24.09.2017 MAJIRA YA SAA 11:00HRS KATIKA MTAA WA LUMALA KATA YA KAWEKAMO WILAYA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTOTO MCHANGA AMBAYE JINA LAKE BADO HALIJAFAHAMIKA MWENYE JINSIA YA KIKE ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA SIKU MOJA AMEOKOTWA KWENYE SHIMO LA CHOO LINALOTUMIKA AKIWA HAI BAADA YA KUTUPWA NA MZAZI ASIYEFAHAMIKA KISHA KUONDOKA KUSIKOJULIKANA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI INADAIWA KUWA BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA TOKA MTOTO ALIPOTUPWA, PALIKUWA NA MTU ALIYEKWENDA KUJISAIDIA CHOONI NDIPO AKIWA CHOONI ALISIKIA SAUTI YA MTOTO MCHANGA AKILIA TOKA NDANI YA SHIMO LA CHOO.  INASEMEKANA KUWA BAADA YA MTU HUYO KUSIKIA SAUTI HIYO YA MTOTO AKILIA, ALIKWENDA KUTOA TAARIFA KWENYE UONGOZI WA SERIKALI ZA MTAA AMBAPO UONGOZI WA MTAA ULIFIKA MAHALI HAPO KISHA ULITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI.
ASKARI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIYO WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WALIOKUWEPO ENEO HILO NA KUFANIKIWA KUTOA KICHANGA HICHO CHA MTOTO TOKA NDANI YA SHIMO LA CHOO KIKIWA HAI. MTOTO AMEPELEWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MSAKO KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA MWANZA, ILI KUWEZA KUBAINI MZAZI/WAZAZI WA MTOTO HUYO AMBAO WAMEFANYA UKATILI HUO DHIDI YA MTOTO, ILI BAADAE WAWEZE KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO NA DAAE IWE FUNDISHO KWA WENGINE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATOA WITO KWA WANANCHI HUSUSANI WAZAZI/WALEZI AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUTENDA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA MTOTO KAMA VYA KUTUPA MTOTO/WATOTO KWANI NI KOSA LA JINAI NA ENDAPO MTU AKIBAINIKA HATUA STAHIKI ZA KIESHERI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE. PIA ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI TUWEZE KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WETU.
KATIKA TUKIO LA PILI,
KWAMBA TAREHE 24.09.2017 MAJIRA YA SAA 08:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA MWAGILIGILI KATA YA NHUNDULU WILAYA YA MISUNGWI MKAO WA MWANZA, KWILOKEJA BONIPHACE, MIAKA 35, MKAZI WA KIJIJI CHA MWILIGILIGILI, ANATUHUMIWA KUMUUA MKEWE AITWAE SHIJA LUCHAGULA, MIAKA 30, MKAZI WA KIJIJI CHA MWAGILIGILI, HII NI BAADA YA KUZUKA KWA UGOMVI KATI YAO ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI KISHA KUMPIGA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI YA MWILI WAKE KISHA KUMNYONGA HADI KUFA NA BAADAE YEYE MWENYE KWENDA KUJINYONGA HADI KUFA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO ALIKUWA AKIMTUHUMU MKEWE KUWA ANATOKA NJE YA NDOA HALI ILIYOPELEKEA KUZUKA KWA UGOMVI WA MARA KWA MARA BAINA YAO. INADAIWA KUWA KABLA YA TUKIO HILO LA MAUAJI KUTOKEA SIKU HIYO MTUHUMIWA ALIAMKA ASUBUHI NA KUFAGIA UWANJA WA NYUMBA YAO KAMA MTEGO WA KUBAINI WATU WANAOKUJA HAPO NYUMBANI KWAKE, KISHA ALIKWENDA KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KAWAIDA.
INADAIWA KUWA  BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA MTUHUMIWA ALIRUDI NYUMBANI, NDIPO AKIWA HAPO NYUMBANI KWAKE ALIONA MATAIRI YA BAISKELI KATIKA UWANJA WA NYUMBA YAKE NDIPO ULIZUKA UGOMVI KATI YAKE NA MKEWE HUKU AKIMTUHUMU MKEWE KUWA ALIKUWA SI MWAMINIFU KATIKA NDOA HAPO NYUMBA KWAKE NA KUPELEKEA KUMPIGA MKEWE HADI KUMUUA NA YEYE MWENYEWE KUJINYONGA HADI KUFA.
POLISI WANAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA VIFO HIVYO, MIILI YA MAREHEMU TAYARI IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, HUSUSANI WANANDOA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO YA NDOA, BALI WAWAHUSISHE WAZEE WENYE HIKIMA NA BUSARA PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI NA  SERIKALI  ILI KUEPUSHA MAJERUHI NA VIFO VYA AINA KAMA HII VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments